Nini maana ya Wagalatia 6:1 inaposema ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’

Nini maana ya Wagalatia 6:1 inaposema ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’

Wagalatia 6:1 ‘Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.

JIBU: Hapa biblia inatupa mwongozo sahihi wa jinsi ya kuwavuta upya ndugu ambao walianguka katika dhambi. 

Tunafundishwa tuwarejeshe katika Roho ya upole, maana yake sio ya kulaumu au ya ukali. Kwamfano utakuta mtu karudi nyuma katika ulevi wake aliokuwa nao mwanzoni.  hapo yakupasa utumie busara kumrejesha upya ili iwe  rahisi tena mtu huyo kugeuka na kutubu, kuliko kutumia ukali mfano kumkaripia au vinginevyo. Ukitumia kauli za lawama au mashtumu, si rahisi kumvuta, kinyume chake zitamfanya achukie zaidi au akasirike.

Lakini pia sehemu ya pili anasema..ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.

. Maana yake ni kwamba hata wewe mwenyewe Unaweza ukajaribiwa na shetani uwapo katika kazi hii ya kuwavuta wengine waliokengeuka katika wokovu. Kwamfano huyo mlevi anaweza akakutukana, halafu wewe ukakasirika, ukaanza kurejesha lugha za matusi kwake kwasababu ya hasira, hapo tayari umeshaanguka katika dhambi.

Baadhi ya watu wa Mungu wamejaribiwa na kuanguka  katika uzinzi walipokuwa wanafanya huduma Kwa watu walio wa jinsia tofauti na wao. Wengine katika anasa waliposhirikiana  na watu wa kidunia waliowashuhudia habari za Yesu.

Hivyo tunapaswa tujichunge nafsi zetu sana tuwapo katika kuipeleka habari njema kwa makundi ya watu tofauti tofauti. Kwasababu na sisi pia shetani anatuwinda. Lakini Tukiwa watu wa maombi na kuliishi Neno tutajilinda sana  nafsi zetu na mitego hiyo ya shetani. Ndio maana ya hilo Neno ‘ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe’.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo

Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?

Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.

NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments