Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Swali: Kwanini Petro na Paulo walishindana na pia tunajifunza nini katika kushindana kwao?.

Jibu: Tusome,

Wagalatia 2:11 “Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu”

Kushindana kunakozungumziwa hapo si kushindana kwa maneno ya dini kule kunakozungumziwa katika 1Timotheo 6:4, 2Timitheo 2:14 na Wafilipi 2:14, kwamba tutende mambo yote pasipo mashindano wala manung’uniko.

Wala si mashindano ya Imani, yale yanayozungumziwa katika Wafilipi 1:30 na Waebrania 12:1 ambayo tunapaswa tuwe nayo, (yaani kushindana dhidi ya nguvu za giza na kuishikilia imani).

Bali neno “mashindano” kama lilivyotumiwa hapo na Paulo lilimaanisha “kukabiliana”. Maana yake Paulo alipofika Antiokia na kukutana na Petro alikabiliana naye uso kwa uso na kumwonya kuhusiana na tabia aliyoonesha ya uvuguvugu juu ya desturi za wayahudi katika kula.

Maana yake Petro alipokuwa ameketi na wayahudi aliungana nao kwa kutokula vyakula vilivyo najisi kwa hofu ya wayahudi…lakini mahali alipoketi katika chakula pamoja na watu wa mataifa, alishirikiana nao katika vyakula hivyo vilivyo najisi kwa wayahudi.

Sasa tabia hiyo haikuwa sawa, ndipo Paulo alipoona na kumkabili na kumwambia dhahiri kuwa anachokifanya sio sawa.

Wagalatia 2:11 “Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu

12 Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.

13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao.

14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?”.

Tunachoweza kujifunza kwa Paulo ni ujasiri wa kusimama kuitangaza kweli pasipo kujali cheo cha mtu wala heshima ya mtu, ikiwa na maana kwamba ikiwa yeyote ananyanyuka na kwenda kinyume na kweli basi anapaswa akabiliwe na kuonywa pasipo kujali cheo chake wala umaarufu wake lakini kwa nia ya upendo.

Vile vile tunachojifunza kwa Mtume Petro ni unyenyekevu, kwani baada ya kuonywa na Paulo alitubu na huoni popote akimkasirikia Paulo zaidi sana utaona anakuja kuwaelekeza watu kwenye nyaraka za Paulo kwamba wazisome..

2 Petro 3:15 “Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa

16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe”.

Na sisi hatuna budi kuiga ujasiri wa Paulo na unyenyekevu wa Petro, huo ndio ukristo!!!..Lakini si kuona dhambi na kuzifumbia macho au kuambiwa ukweli na kukasirika badala ya kujifunza na kubadilika.

Bwana atusaidie katika hayo yote.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments