Home

DenisDevis ByDenisDevis

Hakuna kama Bwana

Related Posts

Yesu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme

DenisDevis ByDenisDevis

njoni kwangu

ninyi nyote msumbukao

DenisDevis ByDenisDevis

mbinguni

ni kule juu

DenisDevis ByDenisDevis

Aponywa Ukimwi.

Jina langu ni Stella Ayong kutoka Buea, Kusini Magharibi mwa Kameruni, Napenda kushudia matendo makuu ya ajabu ambayo Bwana Yesu amenifanyia katika maisha yangu.

Mimi nilizaliwa nje ya ndoa na wazazi wangu mwaka 1973. Ni mtoto wa tatu katika familia, lakini ni binti wa kwanza wa mama yangu, ambaye baadaye alikuja kuolewa , lakini alitelekezwa na mume wake. Mpaka nilipofikisha miaka 13 nilikuwa mshirika wa kanisa la Presbyterians. Lakini kwa wakati huo nilikuwa ni mtukutu sana, mpaka nilipofikisha miaka 15 nilipata mvulana, na kwa kweli nilizini naye mara nyingi kwa muda mrefu sana. Lakini mahusiano yetu yalidumu kwa miaka 5 tu, baada tu ya kipindi fulani nilipoanza kujisikia kuumwa na kupelekwa hospitali. Ambapo niilikaa kule kwa muda wa wiki tatu, lakini kwa muda wote huo niliokuwa hospitali, Yule mvulana hakuwahi kuja kunijulia hali, nilivunjika moyo na kujiuliza ni kwanini anafanya hivyo. Hivyo Kabla sijaondoka hospitali vipimo vyote vya damu vilichukuliwa na majibu yakatoka ila sikupewa mimi bali mama yangu.

Lakini tuliporudi nyumbani nilitamani kujua ni shida gani ninayo, hivyo ikanigharimu niende kupekua karatasi zote zinazohusiana na hospitali katika chumba cha mama yangu, na huko ndipo nilipogundua kuwa kumbe nimethirika na virusi vya UKIMWI. Kipindi hicho nilikuwa ninamiaka  19, kwa kweli nililia sana na kuanza kujiulaumu maisha yangu. Nilielewa sasa ni kwanini Yule mvulana hakuja kunitembelea hospitali, nikizingatia yeye ndiye aliyekuwa mvulana wangu wa kwanza na wa pekee sikuwa na mwingine,  ni wazi kuwa yeye ndiye aliyeniambuza ukimwi. Nilimchukia sana.

Kulikuwa na mtu mmoja mfanyakazi wa ile hospitali niliyopimwa ambaye alilijua tatizo langu, alizichukua habari zangu na kuzitangaza kijiji kizima, mpaka habari ikamfikia Yule mvulana ambaye nilikuwa naye. Na cha kushangaza ni kwamba nilipotoka hospitali bado alikuwa anataka kuja kuzini na mimi, lakini nilikataa kwasababu nilijua kuwa yeye ndiye aliyeniambukiza virusi vya ukimwi.

Wakati huo nilipojindua  kuwa nipo katika hali hiyo , nilianza kulia na kuomboleza juu ya maisha yangu. Japo kipindi hichi nilikuwa simjui Mungu hata namna ya kusali, Lakini nilimwomba Mungu hivyo hivyo, nilimuomba Mungu anisamehe kwa maisha machafu niliyokuwa ninaishi. Na baada ya mwezi mmoja nilienda kwa shangazi yangu kwenye mkoa mwingine. Lakini nilipofika kule nilipata mwanaume mwingine ambaye pia nilifanya naye dhambi ya uzinzi. Baada ya muda tena nilianza kuumwa vibaya sana. Hali yangu ilizidi kuwa mbaya sana.

Shangazi yangu mmoja ambaye ni mhuguzi alinichukua vipimo tena ili kuangalia afya yangu, na kwa mara nyingine nikaonekana ninamaambukizi mpya ya virusi vya ukimwi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2001, nili paralaizi, sikuweza kula au kunywa kitu chochote. Nilikuwa ninalishwa na wengine kwasababu mikono yangu ilikuwa haiwezi kusogea. Nilisaidiwa kupelekwa chooni, nilianza kukohoa sana, na kupata maumivu mengi ya mwilini. Japo nilijua kuwa ni muathirika lakini sikumwambia shangazi yangu jambo hilo kwa muda wa wiki tatu. Nilipopata unafuu kidogo niliondoka kwa shangazi yangu na kwenda kwa mjomba yangu, ambaye alimjua Bwana YESU, na ni mshirika wa Christian Missionary Fellowship International. Huko nilihubiriwa injili na watu mbalimbali, na katika mikutano ya kiinjilisti pia,.

Ndipo Mungu aliponifungua macho yangu na kujiona  mimi ni kama nguruwe. Nilijiona nimeyaharibu maisha yangu, na hakuna tumaini lingine mbele yangu. Nilikuwa nalia sana lakini mjomba wangu ambaye alikuwa ameshampa Bwana maisha yake, alikuwa akinifariji na kuniambia nisigope kwa Mungu yote yanawezekana,. Aliniambia ninachopaswa kufanya ni kutubu tu dhambi zangu zote nilizomkosea Mungu na kuziacha.

Nilimpokea BWANA YESU KRISTO maishani mwangu, na kuanzia huo wakati maisha yangu yalibadilika sana, Niliacha maisha ya uzinzi lakini nilipofikiria jinsi nilivyojiharibu huko nyuma na ya wale watenda dhambi wenzngu nilikuwa ninalia tu, Nilikuwa nikimwomba Mungu rehema kwa yote niliyoyafanya na kwa maisha ya wengine pia niliyoyaharibu.

Mwanzoni nilimchukia sana Yule mvulana lakini kwa jinsi siku zilivyokuwa zinakwenda nikiwa ndani ya Kristo nilianza kumwonea huruma na kuhisi kumsamehe na kumwombea pia.

Ilipofika mwaka 2002 nilisikia kuna mkutano wa maombezi kwa wote walio na ugonjwa wa HIV. Nilisafiri pamoja na kiongozi watatu. Na siku ya mwisho ya mkutano ule mhubiri aliagiza wagonjwa wote wenye HIV waje mbele kuombewa na kuwekewa mikono. Pale mbele palikuwa pamejaa sana, kiasi kwamba kulikuwa hakuna nafasi ya watu kusimama. Mhubiri aliomba viongozi wenzake waje kuhudumu pamoja naye kutuwekea mikono, na tulivyo maliza, tuliruhusiwa turudi kwenye viti vyetu tukae.

Mkutano ulipoisha tulirudi nyumbani, Lakini niliporudi niligundua kuwa zile dalili za ugonjwa hazipo tena ndani yangu. Kikohozi kilipotea, Homa iliondoka,na vipele vikatoweka. Sijawahi kusikia maumivu mingine kuanzia huo wakati na kuendelea. Ndipo mke wa mjomba  yangu alinishauri nikapime ili kuthibitisha uponyaji wangu. Lakini sikwenda kwasababu nilijua kuwa Mungu ameshaniponya.Na cha ajabu ni  kwamba tangu ule mkutano ulipoisha ilikuwa ni mwaka 2002, hadi kufika mwaka 2008, sikuwahi kuwa na dalili yoyote ya kuumwa, sio hata kuumwa kichwa, lakini bado sijaenda hospitali kuthibitisha uponyaji wangu.

Ilipofika April 2008, kaka yangu mmoja alinishauri niende kwenye vipimo, niliamua kwenda japo moyoni mwangu nilijua kabisa Mungu alishaniponya. Hata hivyo niliamka asubuhi na mapema kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo vya ukimwi, mimi ndio niliyekuwa wa kwanza kufika pale, na nikawaambia wahuguzi mimi ni mtu ambaye nilikuwa nimeathirika na ugonjwa wa Ukimwi lakini nilimpa Bwana maisha yangu, na yeye akaniponya na leo  nimekuja hapa kuthibitisha uponyaji wangu kutoka kwake.

Basi Yule mhuguzi akachukua vipimo akaenda ndani, muda kidogo wagonjwa wengine wane walikuwa kwa shida kama hiyo walikuja  na kuniuliza  ni hospitali gani nilikwenda kupima na kuniambiwa kuwa mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi, ndipo nikawaeleza hospitali kadhaa nilizopitia na zote walinieleza kuwa nina virusi vya ukimwi. Ndipo Yule mhuguzi akarudi kunichukua vipimo tena mara ya pili, lakini akaona ni NEGATIVE sina virusi vya ukimwi.

Baada ya hapo wakanilitea kitabu cha Majibu, ndipo  nikapiga magoti pale pale nikimshukuru Mungu, huku nikilia kwa machozi ya furaha. Nesi mmoja akaniinua na kuniambia “MUNGU WAKO, NI MUNGU KWELI WA MIUJIZA”. Aliniambia niende nikamwelezee Daktari hali yangu lakini kwa jinsi nilivyokuwa ninafuraha, Niliondoka na kwenda moja kwa moja kwa mjomba wangu ambaye ni kiongozi wa kanisa. Vile vile nilienda kwa Mhubiri Yule wa Christian Missionary Fellowship International kumweleza ushuhuda wangu. Alifurahi na kuniambia niende mfungo wa siku tatu kumshukuru Mungu kwa kile alichonitendea. Nilianza hilo zoezi haraka siku iliyofuata.

Jumapili iliyofuata niliutoa ushuhuda wangu  kwa kanisa lote. Watu wengi sana walidondokwa na machozi kwa wema ambao amenifanyia, na watu sita katika ya waliowepo kanisani siku ile walimpa Bwana maisha yao. Ninayo furaha sana kwa yale Mungu aliyonitendea katika maisha yangu. Siwezi kuishiwa na shukrani kwake kwa wema wake mwingi juu ya maisha yangu.

Jina lake lihimidiwe milele.

STELLA AYONG.

DenisDevis ByDenisDevis

Ameponywa kansa iliyokuwa katika hatua ya Nne.Hakuna mtu angependa kupokea aina ya taarifa niliyoipokea mimi kwenye simu kutoka kwa daktari wangu.

Daktari Alisema Shirley umetafunwa na kansa sana sio tu kwenye matiti yako bali mpaka kwenye mifupa yako, na viungo vyako vya ndani,na mpaka kwenye tezi zako.

Kwa kweli nililia sana nikajiuliza, hii inawezakanikaje kwani nimekuwa nikimtumikia Mungu maisha yangu yote, nashindwa kuelewa ni kwanini?

Kwa kitambo nimekuwa nikisikia maumivu ya kifua, na kujihisi mdhaifu na vibaya, lakini huwa ni mara chache sana ninakwenda kwa daktari lakini baada ya kuona maumivu yanadumu  kwa muda mrefu hayaishi ndipo nilipoamua kwenda kuangalia afya yangu. Kilichofuata nilichukuliwa vipimo kadha wa kadha, na baadaye ndipo niligundulika kuwa ni Kansa hatua ya nne (stage 4). Hatua hii haitibiki na hivyo niliambiwa nina siku 90 tu za kuishi

Maswali mengi yalianza kupita ndani ya kichwa cha Mume wangu, akiwaambia watu, Itakuwaje kama Shirley akifa leo, watoto wetu watakuwa katika hali gani, mimi nitaenda wapi? Mimi nitafanya nini? Haiwezekani nahitaji maandiko kwasababu hapo ndipo pekee ninaweza kupata faraja..Nilimfuata mke wangu na kumuuliza je! Ni repoti ya nani tunapaswa kuiamini?,Daktari au Mungu? Neno la Mungu linatuambia tutaishi hatutakufa na pia linatuambia hakuna silaha itakayorushwa kinyume chetu itakayofanikiwa, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”

Lakini siku iliyofuata maumivu yalizidi kuongezeka.

Mpaka nikakiri kutembea kwake kumekuwa kwa shida kutokana na mauvivu yaliyo sehemu ya juu ya paja langu, na uvimbe ambao upo katika ziwa langu la kuume, ulio mkubwa kiasi cha nusu ngumi, kwakweli mawazo mengi yalikuwa yanapita kichwani mwangu yakinishawishi ni heri nife kuliko kuishi.

Lakini mimi na mume wangu tuliikataa roho ya hofu, badala yake tulijifunza kuishi kwa imani na bila kutamka neno hata moja la mashaka.

Nilikuwa nikisema kwa ujasiri, sijawahi kuona mahali popote kwenye maandiko,kama kuna mtu alishamfuata Yesu Kristo ili amponywe na akaondoka bila kuponywa, nilianza kufahamu sasa Imani sio tu kuamini kuwa Mungu anaweza kukuponya lakini pia ni kuamini kuwa Mungu atakuponya.

Hivyo niliendelea kutafuta ongozo wa Mungu, nakumbuka siku moja usiku niliamka nikamwona Yesu kwenye pembe ya mwisho wa kitanda changu, na nilipomwangalia hivi niliona, huruma yake, niliona upendo, niliona tumaini,na saa hiyo hiyo Nilianza kuhisi jasho linatiririka sehemu ya nyuma ya goti langu la kulia, ilikuwa sio hali ya kawaida ndipo nikamuuliza Bwana ulikuwa unataka nitoke jasho?

Siku tatu baadaye nilipata jibu pale nilipokwenda kumwona daktari mpya wa masuala ya kansa,Yule daktari akaniambia nina neno moja la kukwambia kabla huaondoka “kwamba unahitaji kutoka jasho”

Alianza kuingia katika tiba ya kusababisha jasho litoke, nilianza kutumia mabafu ya moto na kufanya mazoezi mengi, pamoja na kula  vyakula vya asili, huku marafiki zangu na familia yangu wakifunga na kuomba kwa ajili ya uponyaji wa kiungu, na mume wangu pia akiniombea na kuniwekewa kila mara.

Mume wangu mara kwa mara alikuwa akisema maneno haya  “mtaweka mkono juu ya wagonjwa nao watapata afya, akiamrisha ugonjwa uondoke kwa jina la YESU”

Na wiki tatu mbeleni nilipata ndoto “nilikuwa nimesimama karibu na dirisha la kioo, na ghafla akaona mbele yake semi-trailer kubwa nimejaa mizigo mingi ikija kuelekea upande nilipokuwepo,sikuwa na la kufanya zaidi ya kulia YESU! YESU! YESU!..muda kidogo Lilisimama mbele yangu na kupiga tu kile kioo kilichokuwa mbele yangu..Ndipo nikasikia Roho akizungumza ndani yangu na kusema kuwa lile gari nililolizuia ndio kansa iliyokuwa mwilini mwangu.

Kwa miezi mengine miwili mbeleni niliendelea na matibabu, huku nikiamini Mungu ameshaniponya, Na Kwa jinsi siku zilivyokuwa zinaendelea kwenda ndivyo9 habari njema zilikuwa zinazika zile habari mbaya na siku  ya mwisho nilipokwenda kwa ajili ya vipimo vya siku 90, hatimaye nilipata majibu ya maombi niliyokuwa ninayasubiria kwa muda mrefu.

Daktari aliniambia vipimo vinaonyesha hakuna uvimbe wowote kwenye titi lako na vile vile hakuna dalili yoyote ya kansa katika mwili wako. Kwa kweli ninaamini kuwa kuwa mtu aliyekatika hatua ya NNE ya kansa, halafu kansa imeondoka, huo ni muujiza.

Nilikuwa ninaruka ruka kwa furaha nikimshukuru Mungu sana, kuwa yeye ndiye mrejezi wangu, huku nikishangilia kwa furaha sana

Mume wangu anasema alijisikia uhuru mkubwa sana ndani ya nafsi yake, jinsi Mungu alivyompa nafasi tena ya kuendelea kuwa na mke wake mpaka mwisho wa maisha yao ya hapa duniani.

Tokea huo wakati Agosti 2012, mpaka sasa Shirley hajawahi kuwa na dalili yoyote ya kansa.

Shirley anasema: Nimeponywa leo kwasababu nimeliamini na kulipokea Neno lake, na nililifanya kuwa sehemu ya maisha yangu…Alimalizia na kusema:

Yeye hatazami uso wa mwanadamu, kama alinifanyia na mimi atakufanyia na wewe.

Haleluya!, Hata na wewe msomaji, unaweza ukawa na tatizo pengine kubwa kushinda la Shirley, usikate tamaa Huyu Yesu anayezungumzwa na mabilioni ya watu duniani, yupo kweli kukuhudumia na wewe. Mwamini tu, nawe atakutendea muujiza wako.

×

Powered by WhatsApp Chat

× Karibu tukuhudumie..