Aponywa Ukimwi.

Jina langu ni Stella Ayong kutoka Buea, Kusini Magharibi mwa Kameruni, Napenda kushudia matendo makuu ya ajabu ambayo Bwana Yesu amenifanyia katika maisha yangu.

Mimi nilizaliwa nje ya ndoa na wazazi wangu mwaka 1973. Ni mtoto wa tatu katika familia, lakini ni binti wa kwanza wa mama yangu, ambaye baadaye alikuja kuolewa , lakini alitelekezwa na mume wake. Mpaka nilipofikisha miaka 13 nilikuwa mshirika wa kanisa la Presbyterians. Lakini kwa wakati huo nilikuwa ni mtukutu sana, mpaka nilipofikisha miaka 15 nilipata mvulana, na kwa kweli nilizini naye mara nyingi kwa muda mrefu sana. Lakini mahusiano yetu yalidumu kwa miaka 5 tu, baada tu ya kipindi fulani nilipoanza kujisikia kuumwa na kupelekwa hospitali. Ambapo niilikaa kule kwa muda wa wiki tatu, lakini kwa muda wote huo niliokuwa hospitali, Yule mvulana hakuwahi kuja kunijulia hali, nilivunjika moyo na kujiuliza ni kwanini anafanya hivyo. Hivyo Kabla sijaondoka hospitali vipimo vyote vya damu vilichukuliwa na majibu yakatoka ila sikupewa mimi bali mama yangu.

Lakini tuliporudi nyumbani nilitamani kujua ni shida gani ninayo, hivyo ikanigharimu niende kupekua karatasi zote zinazohusiana na hospitali katika chumba cha mama yangu, na huko ndipo nilipogundua kuwa kumbe nimethirika na virusi vya UKIMWI. Kipindi hicho nilikuwa ninamiaka  19, kwa kweli nililia sana na kuanza kujiulaumu maisha yangu. Nilielewa sasa ni kwanini Yule mvulana hakuja kunitembelea hospitali, nikizingatia yeye ndiye aliyekuwa mvulana wangu wa kwanza na wa pekee sikuwa na mwingine,  ni wazi kuwa yeye ndiye aliyeniambuza ukimwi. Nilimchukia sana.

Kulikuwa na mtu mmoja mfanyakazi wa ile hospitali niliyopimwa ambaye alilijua tatizo langu, alizichukua habari zangu na kuzitangaza kijiji kizima, mpaka habari ikamfikia Yule mvulana ambaye nilikuwa naye. Na cha kushangaza ni kwamba nilipotoka hospitali bado alikuwa anataka kuja kuzini na mimi, lakini nilikataa kwasababu nilijua kuwa yeye ndiye aliyeniambukiza virusi vya ukimwi.

Wakati huo nilipojindua  kuwa nipo katika hali hiyo , nilianza kulia na kuomboleza juu ya maisha yangu. Japo kipindi hichi nilikuwa simjui Mungu hata namna ya kusali, Lakini nilimwomba Mungu hivyo hivyo, nilimuomba Mungu anisamehe kwa maisha machafu niliyokuwa ninaishi. Na baada ya mwezi mmoja nilienda kwa shangazi yangu kwenye mkoa mwingine. Lakini nilipofika kule nilipata mwanaume mwingine ambaye pia nilifanya naye dhambi ya uzinzi. Baada ya muda tena nilianza kuumwa vibaya sana. Hali yangu ilizidi kuwa mbaya sana.

Shangazi yangu mmoja ambaye ni mhuguzi alinichukua vipimo tena ili kuangalia afya yangu, na kwa mara nyingine nikaonekana ninamaambukizi mpya ya virusi vya ukimwi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2001, nili paralaizi, sikuweza kula au kunywa kitu chochote. Nilikuwa ninalishwa na wengine kwasababu mikono yangu ilikuwa haiwezi kusogea. Nilisaidiwa kupelekwa chooni, nilianza kukohoa sana, na kupata maumivu mengi ya mwilini. Japo nilijua kuwa ni muathirika lakini sikumwambia shangazi yangu jambo hilo kwa muda wa wiki tatu. Nilipopata unafuu kidogo niliondoka kwa shangazi yangu na kwenda kwa mjomba yangu, ambaye alimjua Bwana YESU, na ni mshirika wa Christian Missionary Fellowship International. Huko nilihubiriwa injili na watu mbalimbali, na katika mikutano ya kiinjilisti pia,.

Ndipo Mungu aliponifungua macho yangu na kujiona  mimi ni kama nguruwe. Nilijiona nimeyaharibu maisha yangu, na hakuna tumaini lingine mbele yangu. Nilikuwa nalia sana lakini mjomba wangu ambaye alikuwa ameshampa Bwana maisha yake, alikuwa akinifariji na kuniambia nisigope kwa Mungu yote yanawezekana,. Aliniambia ninachopaswa kufanya ni kutubu tu dhambi zangu zote nilizomkosea Mungu na kuziacha.

Nilimpokea BWANA YESU KRISTO maishani mwangu, na kuanzia huo wakati maisha yangu yalibadilika sana, Niliacha maisha ya uzinzi lakini nilipofikiria jinsi nilivyojiharibu huko nyuma na ya wale watenda dhambi wenzngu nilikuwa ninalia tu, Nilikuwa nikimwomba Mungu rehema kwa yote niliyoyafanya na kwa maisha ya wengine pia niliyoyaharibu.

Mwanzoni nilimchukia sana Yule mvulana lakini kwa jinsi siku zilivyokuwa zinakwenda nikiwa ndani ya Kristo nilianza kumwonea huruma na kuhisi kumsamehe na kumwombea pia.

Ilipofika mwaka 2002 nilisikia kuna mkutano wa maombezi kwa wote walio na ugonjwa wa HIV. Nilisafiri pamoja na kiongozi watatu. Na siku ya mwisho ya mkutano ule mhubiri aliagiza wagonjwa wote wenye HIV waje mbele kuombewa na kuwekewa mikono. Pale mbele palikuwa pamejaa sana, kiasi kwamba kulikuwa hakuna nafasi ya watu kusimama. Mhubiri aliomba viongozi wenzake waje kuhudumu pamoja naye kutuwekea mikono, na tulivyo maliza, tuliruhusiwa turudi kwenye viti vyetu tukae.

Mkutano ulipoisha tulirudi nyumbani, Lakini niliporudi niligundua kuwa zile dalili za ugonjwa hazipo tena ndani yangu. Kikohozi kilipotea, Homa iliondoka,na vipele vikatoweka. Sijawahi kusikia maumivu mingine kuanzia huo wakati na kuendelea. Ndipo mke wa mjomba  yangu alinishauri nikapime ili kuthibitisha uponyaji wangu. Lakini sikwenda kwasababu nilijua kuwa Mungu ameshaniponya.Na cha ajabu ni  kwamba tangu ule mkutano ulipoisha ilikuwa ni mwaka 2002, hadi kufika mwaka 2008, sikuwahi kuwa na dalili yoyote ya kuumwa, sio hata kuumwa kichwa, lakini bado sijaenda hospitali kuthibitisha uponyaji wangu.

Ilipofika April 2008, kaka yangu mmoja alinishauri niende kwenye vipimo, niliamua kwenda japo moyoni mwangu nilijua kabisa Mungu alishaniponya. Hata hivyo niliamka asubuhi na mapema kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo vya ukimwi, mimi ndio niliyekuwa wa kwanza kufika pale, na nikawaambia wahuguzi mimi ni mtu ambaye nilikuwa nimeathirika na ugonjwa wa Ukimwi lakini nilimpa Bwana maisha yangu, na yeye akaniponya na leo  nimekuja hapa kuthibitisha uponyaji wangu kutoka kwake.

Basi Yule mhuguzi akachukua vipimo akaenda ndani, muda kidogo wagonjwa wengine wane walikuwa kwa shida kama hiyo walikuja  na kuniuliza  ni hospitali gani nilikwenda kupima na kuniambiwa kuwa mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi, ndipo nikawaeleza hospitali kadhaa nilizopitia na zote walinieleza kuwa nina virusi vya ukimwi. Ndipo Yule mhuguzi akarudi kunichukua vipimo tena mara ya pili, lakini akaona ni NEGATIVE sina virusi vya ukimwi.

Baada ya hapo wakanilitea kitabu cha Majibu, ndipo  nikapiga magoti pale pale nikimshukuru Mungu, huku nikilia kwa machozi ya furaha. Nesi mmoja akaniinua na kuniambia “MUNGU WAKO, NI MUNGU KWELI WA MIUJIZA”. Aliniambia niende nikamwelezee Daktari hali yangu lakini kwa jinsi nilivyokuwa ninafuraha, Niliondoka na kwenda moja kwa moja kwa mjomba wangu ambaye ni kiongozi wa kanisa. Vile vile nilienda kwa Mhubiri Yule wa Christian Missionary Fellowship International kumweleza ushuhuda wangu. Alifurahi na kuniambia niende mfungo wa siku tatu kumshukuru Mungu kwa kile alichonitendea. Nilianza hilo zoezi haraka siku iliyofuata.

Jumapili iliyofuata niliutoa ushuhuda wangu  kwa kanisa lote. Watu wengi sana walidondokwa na machozi kwa wema ambao amenifanyia, na watu sita katika ya waliowepo kanisani siku ile walimpa Bwana maisha yao. Ninayo furaha sana kwa yale Mungu aliyonitendea katika maisha yangu. Siwezi kuishiwa na shukrani kwake kwa wema wake mwingi juu ya maisha yangu.

Jina lake lihimidiwe milele.

STELLA AYONG.

3 thoughts on “Aponywa Ukimwi.”

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *