KITABU CHA UZIMA

by Admin | 17 July 2018 08:46 am07

Kitabu cha uzima ndio kipi?


Ufunuo 20:11-15

11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa KATIKA VILE VITABU, sawasawa na MATENDO YAO.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 

15 NA IWAPO MTU YEYOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA, KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.”

Amina! Tukifuatilia mistari hiyo hapo juu tunaona katika ile siku ya mwisho ya Hukumu Bwana Yesu atakapoketi kuwahukumu wanadamu katika kiti chake cheupe cha enzi, kutakuwa na aina kuu mbili za vitabu: KITABU CHA UZIMA na VITABU VINGINE,. Hapo unaona kitabu cha uzima kinaonekana ni kimoja tu!. Lakini pia kuna vitabu vingine, ikiashiria ni vingi, kwa ufupi  tuvichunguze hivi vitabu ni vitabu gani;

Kitabu cha Uzima ni kipi? Na je! kinafunua nini sasa?

1) KITABU CHA UZIMA:

Kama kinavyojielezea ni kitabu kinachoelezea UZIMA, kama vile kitabu cha hesabati kinaelezea njia za hesabu, kitabu cha jeografia kinaelezea masuala ya kijeografia vivyo hivyo na vitabu vingine vyote. Na tunafahamu vitabu huwa vinagawanyika katika kurasa mbali mbali. Lakini tunaona vitabu vyote hivi tulivyonavyo duniani vinatueleza tu kanuni na mbinu za mambo mengi yahusuyo ulimwengu huu, na tunaona hakuna kitabu chochote ulimwenguni kilichoweza kuelezea UZIMA wa mwanadamu isipokuwa BIBLIA TU!. Kwahiyo kitabu cha uzima kinachozungumziwa hapo ni BIBLIA ambalo ni NENO LA MUNGU.

2) VITABU VINGINE

Tunaona biblia imevitaja kuwa ni vingi, hivi navyo  vinaelezea habari fulani na sio nyingine zaidi ya wanadamu kulingana na biblia inavyosema. Hivi ni VITABU vya wanadamu na kila mwanadamu anacho cha kwake, kikimwelezea maisha yake jinsi alivyoishi hapa duniani kwa muda wote aliopewa hapa duniani kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Na hivi navyo vina ukurasa, ambazo ni hatua unazopitia hapa duniani, Lakini hivi vitabu vyote havina uzima ndani yake, kitabu cha UZIMA ni kimoja tu, na ndio maana hivi vyote vinakitegemea hicho cha UZIMA kutoa hatma ya mwanadamu.

Kwahiyo kile kitabu cha UZIMA kinaelezea kanuni na taratibu za mwadamu anavyopaswa aishi hapa duniani ili aupate huo uzima uliondikwa ndani yake, hivyo basi kama wanadamu tunaoandika vitabu vya maisha yetu tunapaswa tuviandike vifanane na kile  cha UZIMA yaani BIBLIA, kuanzia utoto wetu mpaka kuondoka kwetu duniani vitabu vyetu vinatakiwa vifanane na  cha UZIMA, na huko ndiko KUONEKANA KWA  MAJINA YETU KATIKA KITABU CHA UZIMA. 

Hivyo ndugu kitabu chako unakiandikaje? angalia muda unavyokimbia! usiseme nitampokea Kristo au nitaishi maisha matakatifu nifikisha umri fulani au nikishapata kitu fulani. Jua mpaka sasa kitabu chako kinaendelea kuandikwa na ndivyo kurasa zinavyozidi kufunguka na kufunga, muda unavyozidi kwenda ghafla utajikuta kitabu chako kimefungwa kinasubiriwa kufunguliwa kwenye ILE SIKU YA HUKUMU. 

Na siku ile ya Hukumu kile cha UZIMA kitafunguliwa na cha kwako pia kitafunguliwa, vitalinganishwa, kama vinafanana au la! ‘”HUKO NDIKO KUHAKIKIWA JINA LAKO”. Kama Jina lako halikuonekana inamaanisha kitabu chako (maisha yako), Hayaendani na kile cha UZIMA  (yaani Biblia, NENO LA MUNGU). Hivyo basi kwa kuwa hauna UZIMA ndani yako sehemu yako itakuwa katika lile ziwa liwakalo Moto na kibiriti.

Kama mkristo maisha yetu kila siku tunapaswa tuyalinganishe maisha yetu na biblia, je! tukifanyacho kinaendana na kitabu cha uzima?. unafahamu kabisa waasherati, wazinzi, walevi, watukanaji, waabudu masanamu, waongo, wasengenyaji, mashoga, wasagaji, wavutaji sigara, wafanyaji wa mustarbation, watazamaji wa pornography, waizi, mafisadi,waendaji kwa waganga na wapiga ramli, wala rushwa, wauaji, nk, watu wa dizaini hii maisha yao yapo mbali na kile kitabu cha UZIMA, unategemea vipi uonekane katika kile kitabu, kumbuka majina yanayozungumziwa pale sio John, Yohana au Mary bali ni maisha yako  Jihakiki ndugu komboa wakati siku hizi ni za mwisho. soma. 

Ufunuo 21:27 ” Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”

Siku zote Kitabu hakiandikwi katika siku moja, ili kitabu chako kifanane na kile cha UZIMA Sio hatua ya siku moja bali ya maisha yako ya kila siku, usiishi maisha ya kuidharau injili leo ukasema siku moja nitamgeukia Mungu, usijinganye kile kitabu haukifananishi ndani ya siku moja inahitaji maisha. Bwana YESU alisema

 Luka 9:23″ Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate. ” Unaona sio siku moja.

Maombi yangu ni wewe umgeukie Mungu. Anza kukiandika kitabu chako vizuri katika muda wako wa maisha uliobakiza hapa duniani, kila siku kifananishe kitabu chako na  cha UZIMA ili siku ile ikifika JINA LAKO LIONEKANE. UIEPUKE HUKUMU.

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi 

+255693036618/+255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

KITABU CHA UKUMBUSHO

INJILI YA MILELE.

BARUA INAYOSOMWA

JE! KUNA UBAYA WOWOTE KUWAOMBEA NDUGU ZETU WALIOKUFA KATIKA DHAMBI, MUNGU AWAKUMBUKE KATIKA UFALME WA MBINGUNI?

JE! MUNGU ANAMJARIBU MTU?


Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2018/07/17/kitabu-cha-uzima/