by Admin | 17 July 2018 08:46 am07
Ndoa na talaka, kibiblia ni inakuwaje?
Mathayo 19:3-8″ Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, KWASABABU HIYO, MTU ATAMWACHA,BABAYE NA MAMAYE, ATAAMBATANA NA MKEWE; NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA;
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. BASI ALIOWAUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIWATENGANISHE.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. “
Hapa tunaona jambo la kuachana kwa mke na mume halimpendezi Mungu hata kidogo, kwasababu biblia inasema alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hivyo ndoa haipaswi kuvunjwa isipokuwa kwa sababu zifuatazo zilizohorodheshwa kwenye biblia;
Biblia inasema kwenye
Mathayo 19:9″ Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWASABABU YA UASHERATI, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. “.
Ikiwa mmojawapo kati ya wanandoa amefumaniwa katika uzinzi hapo biblia imeruhusu kumwacha mtu huyo, na kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine, lakini kama ni kwasababu nyingine yoyote tofauti na uzinzi mfano kugombana, kuudhiana, fitna, matatizo, shida, dhiki,magonjwa n.k. hapo biblia hairuhusu kuachana, na hata kama imetokea wameshindwa kulewana na kupelekea kuachana hairuhusiwi kwenda kuoa au kuolewa tena, Biblia inasema kila mmoja akae kama alivyo, ikiwa kama wakipatana wanaweza wakarudiana kinyume na hapo watakuwa wanafanya uzinzi.(marko 10:11-12) ,
Biblia inasema
1Wakoritho 7:10- 11″ Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.
Hivyo basi ikiwa jambo kama hili limetokea mmojawapo kukamwatwa katika uzinzi ni vizuri ukajifunza kusamehe ili ndoa isivunjike, Mungu hapendi kuachana, kwasababu hata Bwana Yesu Kristo anatusamehe sisi mara nyingi pale tunapomfanyia uasherati wa kiroho, je! sisi hatupaswi kufanya zaidi? lakini ikiwa huwezi kuvumilia unaweza ukaivunja utakuwa hauna hatia biblia imeruhusu wewe kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine.
2) IKIWA AMETAKA KUKUACHA KWA SABABU YA IMANI YAKO:
Kama imetokea mlifunga ndoa wakati wote hamjawa waamini, na wewe ukaja kuwa muamini angali ukiwa ndani ya hiyo ndoa, na mkeo/mumeo asitake kukubaliana na imani yako na akaamua kukuacha asiishi tena na wewe, katika hali kama hiyo biblia inaruhusu wewe kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine lakini iwe katika BWANA TU!. Lakini kama ikitokea yule mtu katika hali yake ya kutokuamini anakubali kuishi na wewe hautakiwi kumuacha ukimuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine utakuwa UNAFANYA UZINZI! .
soma…
1Wakoritho 7:12-16 ” Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? “.
Kumbuka kuachana huku ni kwa wale tu! walioana kabla ya kuamini! Biblia haitoi ruhusu yoyote kwa wale walioamini kuachana isipokuwa kwa habari ya uasherati tu, na pia biblia hairuhusu mtu mwamini akaoe/kuolewa na mtu asiyeamini! Hilo ni kosa.
Hivyo basi kama maandiko yanavyosema waebrania 13:4″ Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. “. Ni vizuri mtu unapoingia kwenye ndoa ujue ni jambo la kuheshimika na Mungu hapendezwi na wanandoa kuachana kwasababu yoyote ile! (malaki 2:16 ).
Pale ndoa inapofungwa tu! Mungu anaachilia neema na baraka ya ziada tofauti na mtu ambaye hayupo kwenye ndoa, na pale ndoa inapovunjika kumbuka kuna hasara nyingi, ikiwemo kuzuia baraka za kiroho, watoto unawafanya kuwa kama yatima, unajirudisha nyuma na kuanza safari mwanzo hivyo basi ili kuyaepuka hayo kuwa mwaminifu kwa Bwana na kwa mke/mme wako. Na pia ufanye maamuzi sahihi katika kuchagua mwezi ikiwa kama bado haujaingia kwenye ndoa.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?
NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU SAWASAWA NA KUTOKA 20:5-6?
AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2018/07/17/ndoa-na-talaka/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.