Shetani ni nani?

by Admin | 29 August 2019 08:46 am08

Shetani ni nani?…Tafsiri ya Jina shetani ni ‘mshitaki’ au ‘mchongezi’.  Kazi yake ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu.

Jina lingine la shetani ni “LUSIFA” Maana yake ‘NYOTA YA ALFAJIRI’. (Isaya 14:12) Jina  hili Lusifa aliitwa kabla hajaasi, baada ya kuasi ndio akawa shetani.

Alikuwa ni Malaika wa Sifa (Kerubi) huko mbinguni, alikuwa ni Mzuri kwa mwonekano na mkamilifu katika njia zake zote, aliishi katika taratibu za Mungu, na katika njia za Mungu,  na hivyo akapata heshima kubwa mbinguni zaidi ya Malaika wengi (Ezekieli 28:14).. Alikuwa mkamilifu mpaka siku uovu ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15).

Kwasababu ya uzuri wake Moyo wake ukainuka, akataka kujiinua awe kama Mungu, aabudiwe kama Mungu na kwa ujuzi wake mwingi akawashawishi theluthi ya Malaika mbinguni (1/3) waambatane naye.

Vita, vikali vikatokea Mbinguni kati ya Malaika waliokataa kuungana na Lusifa na malaika waliokubali kuungana naye. Biblia haisema vita hivyo vilipiganwa kwa muda gani, lakini inasema mwisho wa siku lusifa pamoja na malaika wake walishindwa vita vile, na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:7).

Na vita hivyo bado havijaisha, vita vya kwanza vilipiganwa mbunguni, kati ya Malaika walio upande wa shetani na wale walio upande wa Mungu na Malaika waliokuwepo Upande wa Mungu wakavishinda, lakini vita vya pili na vya mwisho vinapiganwa hapa duniani na hata sasa bado vinaendelea..Na vitaisha mwisho wa dunia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1. Je! Ni nani aliyemdanganya shetani?

2. Huduma 10 za shetani sasahivi duniani ni zipi?

3. Mpango wa shetani kwa watoto katika siku hizi za mwisho.

4. Agenda kubwa ya shetani kwa kanisa hili la siku za mwisho

5. Mafundisho ya Mashetani ni yapi katika siku hizi za mwisho?

6. Kazi ya Malaika watakatifu sasa ni nini?

HOME

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/29/shetani-ni-nani/