Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

by Admin | 31 August 2019 08:46 pm08

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kwamba ziwa la moto waliandaliwa shetani na malaika zake,(wale walioasi pamoja naye), kutokana na makosa waliyoyafanya huko nyuma kabla ya mwanadamu kuumbwa, ambapo shetani pamoja na kuonywa na Mungu abaki katika kweli lakini hakutaka, akaandaliwa adhabu hiyo,Na vivyo hivyo wanadamu ambao hawataki kukaa katika ile kweli, wao pia watatupwa katika lile ziwa la moto.

 lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hamchomi shetani au mwanadamu kwenye ziwa la moto kama kuwakomoa au kuwakomesha au kuwalipizia kisasi, hapana! bali Bwana anafanya vile ili kuondoa uovu karibu naye kwasababu yeye ni mtakatifu, ili kuelewa zaidi tafakari mfano ufuatao, Wewe ni msafi hupendi uchafu halafu inatokea kuna uchafu umejitokeza pembeni yako au karibu na makazi yako, uchafu huo unakuletea harufu mbaya, na kichefuchefu, na kukufanya ujisikie vibaya sana, dawa pekee ya kuutoa uchafu huo ni lazima itakuwa ni kuukusanya pamoja na kwenda kuutupa au kuuchoma moto? swali ni je! umeuchoma uchafu huo kwasababu unakisasi nao? au kwasababu unataka kuukomoa? jibu ni hapana!! unauchoma uchafu kwasababu umekaa mahali pasipo stahili na wewe huwezi kuchangamana na uchafu, kwahiyo itabidi utengeneze tanuru ili kuundoa uchafu huo. Kadhalika na Mungu pia, yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu, biblia inasema tutakuwa watakatifu kwasababu yeye Mungu ni mtakatifu

1 Petro 15: 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.

17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.  

Unaona hapo sababu pekee ya Mungu kuuteketeza Roho zote zilizoasi katika ziwa la moto ni kwasababu yeye ni MTAKATIFU na hawezi kuchangamana na uchafu, hawezi kukaa mahali pamoja na uchafu, watu waovu hawawezi kuzirithi ahadi za Mungu, hawawezi kuketi pamoja naye, na kama unavyojua takataka ngumu ndiyo inayochelewa kuteketea zaidi kuliko ile laini kadhalika nafsi iliyojichafua sana na mambo maovu ndiyo itakayoadhibiwa sana kuliko ile iliyojichafua kidogo. 

Luka 12: 47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.

48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”. 

Hivyo adhabu ya shetani haiwezi kuwa sawa na ya mwanadamu, yeye atapigwa zaidi, na adhabu ya aliyeua watu 100 haiwezi kuwa sawa na aliyeua watu 10 n.k Lakini mwisho wa yote roho zote zilizoasi(shetani na wanadamu walioasi) zitakufa katika lile ziwa la moto, kwasababu hazina uzima wa milele, hiyo ndiyo mauti ya pili biblia inayoitaja katika (ufunuo 2:11,ufunuo 20:14). Kwahiyo tujitahidi tumwishie Mungu, tukijua kuwa ipo hukumu mbeleni inatungojea. 

Ubarikiwe sana. . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=DaH7IK-F324[/embedyt]


Mada zinazoendana:

MBONA MUNGU ANARUHUSU WATU WAPATE SHIDA, ILHALI ANA UWEZO WA KUTUEPUSHA?

JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?

NI NANI ANAYETAWALA DUNIA KATI YA MUNGU NA SHETANI?

MUNGU MWENYE HAKI.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/kwanini-mungu-awachome-watu-kwenye-ziwa-la-moto-na-hali-yeye-ndiye-aliyewaumba/