Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Biblia haijaeleza mahali popote ni nani aliyembatiza Yohana mbatizaji, lakini kwa hekima tunaweza kufahamu kuwa yeye naye alibatizwa kama alivyokuwa anawabatiza wengine, kwasababu ni sharti kwanza uwe kielelezo wa jambo ambalo unalifanya ndipo uwafundishe na wengine vinginevyo utakuwa ni mnafki, huwezi kuwatangazia watu uhuru wakati wewe mwenyewe bado upo vifungoniā€¦

Lakini sasa swali linakuja ni nani aliyembatiza Yohana?..Jibu ni kwamba miongoni mwa watu aliwahubiria suala la ubatizo na kuamini, mmojawapo kati yao ndiye aliyembatiza Yohana. Kumbuka suala la ubatizo, halimtilii mkazo sana mbatizaji kama linavyomtilia yule anayebatizwa, nikiwa na maana kuwa mbele za Mungu yule anayebatizwa ndiye mwenye uwezo wa kuufanya ule ubatizo kuwa batili au la, na sio mbatizaji..Na ndio maana tunakuja kumwona Bwana Yesu, yeye hakustahili kubatizwa na Yohana kwasababu yeye ndiye mwenye haki kuliko yeye, lakini yeye alimwambia fanya hivyo kwa sasa, ni kwasababu gani? Ni kwasababu hakukuwa na mwenye haki Zaidi yake atakayeweza kufanya vileā€¦

Vivyo hivyo,na kwa Yohana kwa kuwa hakukuwa na mtu mwingine aliyeupokea ufunuo ule, pengine aliwaambia wale wafuasi wake, wafanye hivi kwa sasa (yaani wambatize), ili atimize haki yote.

Mfano huo huo pia tunaweza kujifunza kwa Ibrahimu, Mungu alipompa ufunuo wa TOHARA kwa uzao wake wote, na Mungu akamwambia awatahiri watoto wake na watu wa nyumbani mwake,. Tunaona pia yeye naye hakujitenga kana kwamba haumuhusu hapana, bali yeye baada ya kuwatahiri watu wake, kadhalika yeye naye akatahiriwa na wao. soma

Mwanzo 17: 23 “Ibrahimu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
24 Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake.
25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.
26 Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe”.

Unaona hapo sasa kwa mifano hiyo hiyo tunaweza kufahamu kuwa Yohana naye baada ya kumbatiza mmoja wa wafuasi wake, yeye naye akabatizwa na wao, ili haki yote itimizwe, Amen.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/yohana-mbatizaji-alibatizwa-na-nani/