by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09
SWALI: Watu hawa wanao mtumaini shetani na kupata utajiri na Mali, shetani anavitoa wapi?, Na wakati Neno linasema Mali na fedha na dhahabu ni vya Mungu?, Wakolosai 1 :16-17 je shetani anavichukuaje kwa Mungu na kuwapa watu hawa, ingali yeye hana vitu?Je! shetani ana Mali, fedha na dhahabu anavyowapa watu wanaomwabudu?.
JIBU: Ni kweli fedha na dhahabu ni mali ya Bwana (Hegai 2:8). Lakini swali ni kwa namna gani shetani anamiliki fedha? Kama fedha yote ni mali ya Bwana.….Tofauti na watu wengi wanavyofikiri kuwa shetani anakiwanda cha kutengeneza fedha mahali Fulani kuzimu na hivyo mtu akitaka anakwenda kuzimu na kupewa kitita Fulani kama begi na hivyo akirudi huku duniani anakuwa Tajiri ghafla…… lakini kiuhalisia shetani hamiliki mali kwa namna hiyo. Hakuna kiwanda chochote kuzimu cha kutengeneza fedha, wala hakuna fedha zozote zinazofichwa kuzimu…..
Mfumo wa shetani wa kumiliki fedha na mali upo hapa hapa duniani na unatenda kazi hivi;…shetani anawaingia watu wake (wanaweza kuwa wachawi au watu waovu) na kuwashawishi kutengeneza mfumo au taasisi fulani ambayo ni ya kishetani ambayo kwa kupitia hiyo ataweza kukusanya fedha nyingi…ndio hapo kwa kupitia watu wake wadogo atawashawishi watengeneze vitu kama Bar, Casino, sehemu za anasa na starehe n.k ambazo kwa kupitia hizo atawarushia watu mapepo waende kwenye hivyo vitega uchumi! Na hivyo huyo mtu kupata faida Fulani ya haraka kwa kupitia hiyo kazi ya kishetani!…sasa Hizo fedha au mali mtu atakayopata kupitia hiyo taasisi ya kishetani ndio fedha ambazo kapewa na shetani.
Sasa kwa watu wakubwa na wasomi, hatawapeleka kwenye biashara ndogo ndogo hizo, atawaingiza kwenye mitandao yake mikubwa Zaidi labda biashara za madawa ya kulevya, na makampuni ya utengenezaji wa pombe na sigara, ambayo hayo yanatengeneza faida kubwa sana duniani kutokana na wanunuzi wake kuwa wengi….
Na haishii hapo tu! Anakazana kila siku kukusanya utajiri wa ulimwengu kwa nguvu zote, kila siku anatafuta njia ya kuvuta fedha nyingi na mali nyingi kuzipeleka kwenye taasisi zake hizo. Na anabuni taasisi mpya kila siku na kuzianzisha hapa hapa duniani…Na anatafuta viongozi wa serikalini wa juu na wa kidini kuwaweka kama viongozi na waongozaji wa taasisi zake hizo, na ili kazi zake ziende vizuri… Sasa endapo mtu wa kawaida akienda kuomba kazi katika mojawapo ya hizo taasisi zake anampa mtu huyo masharti Fulani na endapo akikubaliana nayo ndio anapata kazi na akikataa anaikosa…ndio hapo kama ni mwanamke ataambiwa pengine aanze kuvaa kikahaba, au aachane na mume wake na aolewe na mshirika wa hiyo taasisi nk..
Na kuna sehemu nyingine na mashirika mengine ambayo huwezi kupata nafasi ya kazi au fursa mpaka umekuwa mshirika kamili wa kikundi hicho. Na utakitambuaje kuwa ni kikundi cha kichawi? Ni pale utakapoona unapewa masharti Fulani pengine ya kutoa kutoa kafara, kuabudu vitu usivyovijua au kulazimishwa kusema maneno fulani…sasa ukishajiunga kwenye kikundi chao basi wanakuajiri na kukupa mshahara mkubwa, sasa hizo fedha mtu atakazozipata kutokana na kazi hiyo ya kishetani ndio fedha za kishetani zenyewe hizo, ambayo shetani alishaziwekeza kupitia hayo mashirika yake maovu. Na anampa yeyote kwa jinsi atakavyo.
Lakini hana kiwanda cha kutengeneza fedha. Na kuna sehemu nyingine na mashirika mengine ambayo huwezi kupata nafasi ya kazi au fursa mpaka umekuwa mshirika kamili wa kikundi hicho. Na utakitambuaje kuwa ni kikundi cha kichawi? Ni pale utakapoona unapewa masharti Fulani pengine ya kutoa kutoa kafara, kuabudu vitu usivyovijua au kulazimishwa kusema maneno fulani…sasa ukishajiunga kwenye kikundi chao basi wanakuajiri na kukupa mshahara mkubwa, sasa hizo fedha mtu atakazozipata kutokana na kazi hiyo ya kishetani ndio fedha za kishetani zenyewe hizo, ambayo shetani alishaziwekeza kupitia hayo mashirika yake maovu. Na anampa yeyote kwa jinsi atakavyo.
Lakini hana kiwanda cha kutengeneza fedha. Na baadhi ya mashirika mengine yanayobeba utajiri mkubwa wa shetani ni mashirika yote ya betting, mashirika ya kutengeneza vipodozi, mashirika ya Rotary, mashirika ya Samaritani, mashirika ya kutengeneza filamu, na MASHIRIKA YA DINI ZA UONGO na kuna dini ambazo ukikubali kujiunga tu kwa tamaa ya kulipwa mshahara na kufuata taratibu zao utapewa misaada mikubwa ambayo gharama zake hutajua zilipotoka…atapata na fursa na channels nyingi, lakini kumbe unatumika katika ufalme wa giza…. kwahiyo pia ni muhimu kabla ya kuingia kwenye shirika Fulani kufanya kazi ni vizuri kulitathmini kwanza shirika hilo au kampuni hilo, misingi yake ni nini? Pia mshirikishe Mungu katika maamuzi yako..
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/shetani-anatolea-wapi-fedha-angali-tunajua-fedha-na-dhahabu-ni-mali-ya-bwana/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.