Tunaposema tuishi kwa Neno, Inamaanisha tuishi maisha ya namna gani?

by Admin | 3 September 2019 08:46 pm09


JIBU: Kuishi kwa Neno ni sawa mtu aseme ishi Kwa sheria au katiba ya nchi.Sasa unaishije kwa sheria ya nchi?, kwanza ni lazima uzijue sheria zenyewe kisha uziishi bila kuzivunja kwa namna yeyote ile, sheria ya nchi inasema usiibe mali ya mwingine, usiue, usile rushwa, usifanye biashara isiyo halali n.k unapozitii hapo ni sawa na kusema unaishi kwa sheria za nchi.

Na maana ya pili ya kuishi kwa sheria za nchi ni kuitumia sheria hiyo hiyo kupata haki yako..Kwamfano mtu haruhusiwi kukutesa, kwasababu sheria inakataza hilo, hivyo unatumia sheria kumshitaki au kumwonya, mtu anayetaka kukudhulu haki yako, kukudhalilisha, kukutapeli, au kukuua, au kukuibia unatumia sheria hiyo hiyo kujilinda…Kwasababu usipoijua haki yako utaonewa.
Na kwenye Neno la Mungu ni hivyo hivyo, unaishi kwanza kwa kulitii Neno la Mungu, Neno linaposema usizini, unapaswa usizini, linaposema mwanamke avae mavazi ya kujisitiri unapaswa ujisitiri, usiabudu sanamu, mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, nguvu zako zote na akili zako zote na jirani yako kama nafsi yako..Yote hayo unapaswa uyatii bila shuruti, Na hapo utakuwa umeishi kwa Neno. Hiyo ni namna ya kwanza.


Namna ya pili pia unalitumia Neno hilo hilo kujilinda dhidi ya yule mwovu, na kudai haki yako… mwovu akija na kusema utakufa wewe unasema Neno linasema sitakufa bali nitaishi (Zaburi 118:17), akija tena na kusema hutapona wewe unasema Neno linasema “kwa kupigwa kwake sisi tumepona (Isaya 53:5)”, unapopita katika bonde la mauti na misukosuko na dhoruba unasema Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu n.k. hivyo tu!..Kwa kufanya hivyo utaishi na wala hakutakuwa na jambo lolote litakalokushinda hapa duniani.
Hiyo ndio maana ya kuishi kwa Neno.


Ubarikiwe!


Mada Nyinginezo:

BIBLIA INASEMA USIONGEZE WALA USIPUNGUZE NENO LA MUNGU, HUKO KUONGEZA NA KUPUNGUZA KUKOJE?

AYUBU ALIJARIBIWA KWA MUDA GANI?

WAPUNGA PEPO WANAOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NI WATU WA NAMNA GANI?

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

NYOTA YA ASUBUHI.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/03/tunaposema-tuishi-kwa-neno-inamaanisha-tuishi-maisha-ya-namna-gani/