Wapunga Pepo wanaozungumziwa kwenye biblia ni watu wa namna gani?

Wapunga Pepo wanaozungumziwa kwenye biblia ni watu wa namna gani?

SWALI: Tukisoma Matendo 19:13 Inasema pale “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, NAO NI WAPUNGA PEPO….” swali,Naomba kufahamu hawa Wapunga Pepo ni watu wa aina gani ndugu zangu?

JIBU: Tafsiri ya Neno kupunga pepo ni kufukuza pepo…hiyo ni lugha iliyotumika katika tafsiri yetu ya Kiswahili inayosimama badala ya kufukuza pepo…Kwahiyo zamani na hata sasa zilikuwepo njia nyingi za kuondoa pepo ndani ya mtu…

Watu wa Mungu wanao uwezo wa kufukuza mapepo kwa kutumia jina la YESU, kadhalika na watu wa shetani wanauwezo wa kufukuza pepo.
Sasa njia wanayotumia watu wa Mungu kufukuza mapepo ni tofauti na njia wanazozitumia wachawi au waganga…

Wakristo wanafukuza pepo na kumfanya yule mtu kuwa huru kabisa kabisa, kwa kutumia jina la Yesu Kristo kwa Imani, mtu huyo anafunguka na kuwa huru..kama mtu alikuwa na pepo fulani lililomletea ugonjwa Fulani labda ugonjwa wa kuumwa tumbo, linapoondolewa kwa jina la Yesu linaondoka moja kwa moja pamoja na ule ugonjwa wake na madhara yake yote.

Lakini waganga wa kienyeji au wachawi wanavyofukuza mapepo ni tofauti kabisa kwao haiwi hivyo..wao hawayafukuzi bali wanaleta mapepo mengine juu ya yule mtu yenye nguvu zaidi ya lile pepo lililopo ndani ya yule mtu, kwahiyo kinachotokea labda yule mtu alikuwa na pepo fulani lililomletea ugonjwa fulani labda wa kuumwa tumbo, Yule mtu anapokwenda kwa mganga (mpunga pepo)… yule mganga anamtumia pepo lingine lenye nguvu kuliko lile la ugonjwa wa tumbo linamwingia labda tuseme pepo la utasa na lile pepo la ugonjwa wa kuuma tumbo nguvu zake zinafunikwa na lile lingine la utasa lililomwingia.

Kwahiyo yule mtu baada ya kuaguliwa na yule mganga anaweza akajisikia unafuu wa kupona tumbo kwa muda…lakini baada ya kipindi fulani anakuja kujigundua tena kapata utasa au ugonjwa mwingine mkubwa zaidi…sasa hiyo hali ya kupunguza pepo hili nguvu kwa kulileta lingine lenye nguvu zaidi ya lile la kwanza ndiyo inayoitwa “kupunga pepo”.

Ni sawa kuleta nyoka ndani ili ale panya wanaokula mahindi yako ghalani, atawapunguza tu na kufurahi kwa muda lakini hawezi kuwamaliza wote, na zaidi ya yote huyo nyoka siku moja atakuletea madhara na wewe…

Kwahiyo waganga hawana uwezo wa kutoa mapepo, wanaongeza pepo juu ya pepo, kwasababu shetani hawezi kujifitini kwenye ufalme wake mwenyewe kama Bwana Yesu alivyosema…

Mathayo 12:26 “Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?”.

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?

UTEKA ULIOGEUZWA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Abisai
Abisai
2 years ago

Naomba hayo masomo yazidikunijenga ktk wokovu, mbarikiwe, namba ya ngu ya whasapu 0710804156

Roden Mbangala
Roden Mbangala
2 years ago
Reply to  Admin

Naomba mnitumie masomo yenu nimeyapenda sana. Namba yangu ni 0756 696 209