KUOTA UMEBEBA MTOTO.

by Admin | 10 October 2019 08:46 pm10

Sehemu kubwa ya ndoto tunazoziota mara kwa mara huwa hazitokani na Mungu wala shetani bali zinatokana na sisi wenyewe..

Na hizi huathiriwa aidha na shughuli tunazozifanya kila siku, au mazingira yanayotuzunguka, Kwamfano, ikiwa wewe ni kondakta wa magari, na kazi ndio hiyo unayofanya kila siku, basi tarajia kuwa ndoto utakazokuwa unaota mara kwa mara zitahusiana na ukondakta utajiona unapiga debe, au upo kwenye magari,, au kama wewe ni mkulima ambaye mara zote  unashida mashambani, tazamia pia ndogo zako nyingi usiku zitahusiana sana na mambo ya mashambani,..

Na vivyo hivyo, ndoto nyingine nyingi kama hizo zinakuja kutokana na shughuli mtu anazozifanya mara kwa mara..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.”

Vile vile ndoto nyingine huja kutokana na mabadiliko ya mwili yetu, kwamfano ikiwa jana usiku ulilala bila kula, tazamia kuwa usiku utaota ndoto zinazoendana na vyakula vyakula aidha unakula lakini hushibi, au unakunywa, au kama ulilala ukiwa umebanwa na mkojo, tarajia kuwa usiku utaona unakojoa mara kwa mara n.k.

Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.”

Hivyo ndoto za namna hii zinawapata watu wengi wakidhani kuwa wameoteshwa na Mungu au shetani kumbe ni ubongo wao ndio umewaotesha, nataka nikuambie sio kila ndoto ni ya kuitilia maanani, ndoto za namna hii zikikujia zipuuzie tu.. kwasababu huwa hazibebi tafsiri yoyote yamaana ya rohoni.

Kama hujafahamu bado kuzitofautisha ndoto unazoziota zinadondekea katika kundi lipi..basi Pitia kwanza hili somo kisha ndio tuendelee..>>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?

Sasa Ikiwa ndoto uliyoota unaamini haitokani na mwili wako, inakupa utata mwingi na huwa inajirudia mara kwa mara, basi lipo jambo unapaswa ujue hapo.

Kumbuka Sikuzote kitu kinachobebwa  ni mzigo, lakini tatizo sio mzigo bali ni mzigo wa aina gani umebebwa, kwamfano kuna kuota umebeba maiti, au kuota umebeba mbao, au kuota umebeba jeneza unatembea  nalo,  hapo ndipo unapopaswa kuangalia sana hicho kilichobebwa ni nini…kwasababu vyote hivyo vinaeleza hali ya mtu ilivyo rohoni.

Sasa kama umeota ubeba mtoto,  na upo ndani ya Kristo fahamu kuwa mtoto ni jukumu, na jukumu lenyewe linahusiana na uleaji. hapo ni Mungu anakuonyesha kuwa kuna jukumu amekupa, au kama halipo sasahivi basi jiandae kukutana nalo hivi karibuni..Inaweza ikawa kwenye huduma yako ya utumishi, au familia yako, au kazini kwako, au popote pale ulipo..

Hivyo unachopaswa kufanya ni kutokulalamika, unapokutana na vizuizi, wala usikasirike mambo kama hayo yakujiapo, ongeza uhusiano wako kwa Mungu. Kwasababu jukumu ni ukomavu. Inawekana Mungu amekupa watu wa kukaa chini yako, hivyo usiwachukie na kuwaona ni mzigo, kaa nao, hujui pengine Mungu ameweka Baraka zako kwako kwa kupitia hao. Au wanakutegemea wewe uwape msaada ya kiroho usiwakatae wala usikwepe hilo jukumu, hujui mbeleni watakuja kuwa nani kwako na kwa wengine..Ndivyo ilivyokuwa kwa Mariamu, hakukataa kumbeba mtoto Yesu pepote alipoambiwa aende, lakini leo hii tunajua ni jinsi gani Bwana Yesu amempa Heshima kubwa.

Mathayo 2:12 “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.”

14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;

15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.”

Lakini kama unajijua upo nje ya Kristo fahamu pia, Mungu anakukumbusha, unabeba jukumu ambalo halitakuwa na faida kwako mbeleni.

Lakini Pia kama unaota umebeba kitoto kisichoeleweka, kibwengo si kibwengo, kama kinakuwekea mzigo mzito usioweza kuubeba, kinakukosesha raha, basi ujue hilo ni pepo, linasimama nyuma yako kukukawiisha katika safari yako ya wokovu hapa duniani, unachopaswa kufanya ni kudumu katika maombi, ombea kila eneo ulilopo, na kila jambo unalolifanya, ili kufunga milango yote shetani anayoweza kuitumia kukurudisha nyuma..

Vile vile kama unaota unabeba jeneza fahamu hiyo ni ishara kuwa unaenda kujiangamiza mwenyewe, hivyo angalia maisha yako, kama upo nje ya Kristo tubu haraka sana na anza kuishi au kufanya mambo yanayompendeza yeye katika eneo ulilopo.

Bwana akubariki.

Group la whatsappJiunge na Group letu ya whatsapp, la masomo ya kila siku kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

MTETEZI WAKO NI NANI?

VITA BADO VINAENDELEA.

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

MAFUNUO YA ROHO.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/10/kuota-umebeba-mtoto/