Je unaweza usisamehewe hapa duniani na kule ukasamehewa?

by Admin | 4 November 2019 08:46 pm11

SWALI: Ukisoma Mathayo 12:32 “utaona anae mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa sasa na hata ule ulimwengu ujao.

Sasa sio ndio kusema, kama nimekufa nikiwa na baadhi ya makosa nitasamehewa ule ulimwengu ujao? Naomba kueleweshwa zaidi”.

JIBU: Mtu anaweza asisamehewe hapa duniani lakini kule aendako akasamehewa…kwamfano yule mnyanganyi aliyesulubiwa na Bwana Yesu pale msalabani, hakusamehewa adhabu ya kifo pale msalabani pengine alimwomba Mungu kimoyo moyo asife pale msalabani, lakini haikusaidia kufa alikufa……

lakini baada ya kufa alisamehewa adhabu ya moto wa milele..ingawa hakusamehewa adhabu ya kuchapwa na mijeledi na kusulubishwa…..lakini Bwana alimwambia atakuwa pamoja naye peponi siku ile kwasababu alitubu…

Mfano mwingine ni wafungwa, wapo wafungwa waliofungwa kutokana na makosa waliyoyafanya kihalali kabisa ambao wametubu na kulia Mungu awafungue kwenye vifungo hivyo…

Lakini Mungu hajawafungua kwenye vifungo vyao mpaka wanakufa..hao hawajasamehewa adhabu hapa duniani lakini wakifa watakwenda paradiso kwasababu walitubu.(Kundi lote hilo ndio kundi la watu ambao hawajasamehewa hapa lakini kule watasamehewa).

DHAMBI ZA MAKUSUDI.

Vilevile ikiwa mtu alishaokoka halafu akaenda kufanya dhambi za makusudi, kwamfano ya uzinzi, baadaye akatubu, biblia inasema mtu kama huyo ni ngumu sana kusamehewa hapa, ni rahisi kukutana na adhabu ya mauti hata kama huko aendako atasamehewa. Hivyo ni kukaa mbali na dhambi..

1Wakorintho 5:1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;

5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

Na pia inawezakana mtu asisamehewe hapa duniani na huko aendako pia asisamehewe..mfano mzuri ni Yule mnyanganyi wa pili aliyesulubiwa na Bwana Yesu pale msalabani, aliyemkufuru Bwana Yesu, Yule hakusamehewa hapa na kule hakusamehewa kwasababu hakutubu.

Lakini sio kama inavyotafsiriwa sasa na baadhi ya imani kwamba kuna uwezekano wa mtu aliyekufa bila kutubu akasamehewa huko anakokwenda kwa kupitia Toharani! hakuna kitu kama hicho mtu yeyote aliyekufa bila kutubu hakuna kusamehewa huko aendako. Atakwenda kuzimu kama maandiko yanavyosema, na hakuna maombi yoyote yatakayoweza kumtoa huko..

Kwahiyo ni heri kutokusamehewa hapa lakini huko uendako ukapata msamaha, na msamaha huo mtu anaupata kwa kutubu tu kabla ya kufa, na si njia nyingine yoyote.

Ubarikiwe.


MADA NYINGINEZO:

KUOTA UMEPOTEA.

INJILI NI NINI?

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/11/04/je-unaweza-usisamehewe-hapa-duniani-na-kule-ukasamehewa/