Je kuzalishwa na mkunga wa kiume ni dhambi?

by Admin | 14 December 2019 08:46 am12

Je kuzalishwa na mkunga wa kiume ni dhambi?..Je Mungu anaweza kutumia chochote kupitisha uponyaji wake?..Je jina la Yesu Kristo lina nguvu ya kuponya kabisa bila kutegemea daktari?

Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa tatizo lolote au ugonjwa wowote ambao mtu anaweza kuupata..Mungu anauwezo wa kuuondoa pasipo mkono wa mwanadamu yoyote kuhusika…Na hiyo inatokana na Imani mtu aliyonayo kwa Mungu..Ukiamini kwa moyo wako wote, basi yote yanawezekana.

Lakini pamoja na hayo..pia Mungu anaweza kutumia chochote kupitisha uponyaji wake…Anaweza kumtumia mwanadamu, anaweza kutumia chakula au chochote kile.

Mtu anaweza akaugua akala aina fulani ya chakula akapona..sasa kiuhalisia sio chakula kilichomponya bali ni ule uponyaji Mungu aliouweka ndani ya kile chakula ndio uliomfungua…

Kadhalika anaweza kumtumia mwanadamu kumponya mtu…anawapa maarifa fulani wanadamu ambayo kwa hayo mtu anaweza kupata uponyaji kwamfano..Mtu anaweza kuugua ugonjwa fulani..labda uvimbe umeota tumboni…na madaktari wakahusika katika kuuondoa uvimbe ule kwa njia ya OPERATION na mtu akawa mzima kabisa.,Sasa hiyo ni nguvu ya uponyaji Mungu aliyoiweka kwenye maarifa ya wanadamu n.k

Sasa tukirudi katika suala la Wakunga wa kiume (kuzalishwa na mkunga wa kiume)

Ni wazi kuwa nyakati za zamani sana hakukuwepo kabisa kwa wakunga wa kiume…au kama walikuwepo walikuwa wachache sana..Lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda wanaongezeka sana..Hiyo ni kutokana na matatizo ya wanawake kuongezeka…Magonjwa ya wanawake yanapozidi kuongezeka madaktari nao wanalazimika kuongezeka na idadi kubwa madaktari wanaoongezeka ni wanaume…Hivyo wanaume wengi wanajikita kuingia kusomea mfumo wa kibaolojia wa mwanamke zaidi ya wanawake wenyewe..huku wanawake wakiwa wachache kutokana na sababu mbalimbali.

Kwasababu hiyo basi sio dhambi kuwepo kwa madaktari wa kiume katika kushughulikia matatizo ya wanawake pale wanawake wanapokosekana kwasababu..lengo la wao kuwepo sio kuongeza matatizo bali kupunguza. Hakuna mtu yeyote anayekwenda hospitalini asiyekuwa na tatizo lolote, wote wanaokwenda wanakwenda kutafuta msaada.

Hivyo kuzalishwa na mkunga wa kiume sio dhambi wala kufanyiwa operation na mwanamume sio dhambi..Zipo operation za uzazi, ambazo kizazi kinalazimika kuchanwa kuondolewa ugonjwa usiopaswa kuwemo humo..Na operation kama hizo huwa zinamlazimisha mgonjwa kuvuliwa nguo zote na kuwa kama alivyozaliwa ili matibabu hayo yaweze kufanyika..na madaktari bingwa wanaofanya hizo operation wengi ni wanaume wakiwa pamoja na manesi wa kike…Hivyo kwa mgonjwa wa kike kutibiwa kwa viwango hivyo  na daktari wa kiume sio dhambi..wala wa kiume pia kutibiwa kwa viwango hivyo na daktari wa kike ambavyo vitamlazimisha kuwa tupu kabisa mbele ya matatibu sio dhambi…Kwasababu lengo ni kupata matibabu na si kitu kingine.

Na matibabu kama hayo yanafanyika  kwa madaktari wa hospitalini tu kwasababu wengi wakiwa katika vyumba vya uchunguzi au operation wanakuwa zaidi ya daktari mmoja tena wa jinsia tofauti, ili kuzuia uzalilishaji na vitu kama hivyo…. na sio kwa waganga wa kienyeji…wala kwa madaktari binafsi wa mitaani ambao wanakuita tu binafsi na kukwambia uvue hichi au kile wakuchunguze..Hao kwa namna yoyote hawapaswi kuruhusiwa kufanya uchunguzi au matibabu ya namna hiyo.

Lakini yote katika yote..Bwana Yesu ndiye mponyaji mkuu..operesheni wakati mwingine zinafeli pamoja na gharama zake zote hizo kubwa…lakini Yesu Kristo hajawahi kushindwa…

Vyakula wakati mwingine vinashindwa kutuponya lakini Yesu Kristo hajawahi kushindwa..Yapo magonjwa ambayo madaktari hawayaelewi chanzo chake lakini Yesu Kristo anayajua.

Madaktari wanatibu kwa gharama kubwa za fedha, na wakati mwingine gharama za kutolewa nguo zote, au nywele zote au kiungo fulani kukatwa ndipo matibabu yaweze kufanyika..lakini Yesu Kristo anafanya bila hayo yote.

Ikiwa unaumwa ugonjwa wowote ule..Nataka na unakaribia kwenda kwenye operesheni…nataka nikuambie Yesu Kristo anaweza kukuponya kabla hujamkaribia  huyo daktari..

Weka mkono mahali unapoumwa..kama ni kifuani, kichwani, tumboni..kama ni ugonjwa ambao huelewi chanzo chake weka kichwani…Yesu anajua chanzo chake..

Sasa baada ya kuweka kichwani..unaposoma sala hii ugonjwa wako unakwenda kuhama sasahivi na kutoweka kabisa..Amini tu.

“Bwana Yesu namwombe mtu ambaye simjui ni nani, wala jina lake, wala ugonjwa wake wala mahali alipo, lakini wewe unamjua jina lake, mahali alipo na tatizo alilonalo..namwombea kwa Imani katika jina lako  lenye nguvu (Jina la Yesu). Kwamba kila ugonjwa na kila pandikizo lililopandikizwa ndani yake na yule adui likapate kutoweka sasahivi katika JINA LA YESU KRISTO! Amen”.

Ikiwa umeisoma hii sala niliyokuombea…Huo ugonjwa umeshaondoka na kama ugonjwa huo ulivyoondoka ndani yako…Ugonjwa wa rohoni pia unapaswa uondoke pia..Na ugonjwa wa rohoni ni dhambi.

Hizo zinaondoka ndani yako kwa kumkiri sasa Yesu Kristo ambaye amekuponya ugonjwa wako..Na baada ya kumkiri kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako..mwambie akusamehe dhambi zote ulizowahi kuzitenda huko nyuma…na wewe mwenyewe dhamiria kuziacha…kama ulikuwa ni mwasherati..umeona utukufu wa Mungu..hivyo usifanye uasherati tena…vivyo hivyo na dhambi nyingine zote. Usizifanye tena,  yasije yakakupata mabaya kuliko hayo uliyokuwa nayo.

Na baada ya kutubu haraka sana nenda katafute ubatizo. Kumbuka ubatizo sahihi ni wa muhimu sana. Na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo.(kulingana na Matendo 2:38). Na Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakuongoza na kukutia katika kweli yote.

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali share na wengine.


Mada Nyinginezo:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Vichwa saba vya mnyama wa kwenye Ufunuo 13 na 17, Ni nini?

JE! MUNGU NI NANI?

Biblia ni nini?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/12/14/je-kuzalishwa-na-mkunga-wa-kiume-ni-dhambi/