Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?

by Admin | 16 December 2020 08:46 pm12

Zaburi 32:9 :Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. KWA MATANDIKO YA LIJAMU NA HATAMU Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia:.


Hatamu ni kifaa, kinachotumika kumwongozea farasi, ikijumuisha ule mkanda unaoshikilia kichwa, na ile kamba inayokwenda moja kwa moja kwa mwongozaji farasi. Kazi ya hatamu ni kumwongoza farasi, na kumpa balansi wakati wa kumwendesha, Tazama picha chini

hatamu

Lijamu ni kifaa kidogo, ambacho huwa kinapitishwa katikati ya midomo wa farasi, hichi kinashikiliwa na Hatamu yenyewe, kazi yake ni kuongeza  Presha kwa mnyama, ikivutwa sana mwendo wa farasi unaongeza, ikivutwa kidogo mwendo unapungua..lijamu ndio inayoeleza mwendo wa farasi. Tazama picha chini;

lijamu

Hivyo Hatamu na lijamu vyote vinafanya kazi pamoja, kumwendesha na kumwongoza farasi.

lijamu na hatamu

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi baadhi,

Yakobo 3:3 “Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.

4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.

5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana”.

Zaburi 39: 1 “Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu”.

Soma pia Mithali 26:3, Isaya 37:29

Hivyo kulingana na vifungu hivyo unaweza kuona tunaonywa tuvichunge vinywa vyetu, tuviweze, tuvitawale, na sio vitutawale sisi. Tutie lijamu, ikiwa na maana kuwa si kila habari ya usengenyaji na sisi tuwepo, si kila maneno yasiyo na maana na sisi tuyachangie, si kila maneno ya laana na sisi tuyatamke. Tunapaswa tujifunze chagua ni kipi cha kuchangia na kipi cha kukaa kimya. Kwasababu ulimi ni kama moto.

Lakini pia tukirudi katika kitabu cha Ufunuo tunaona, siku ile, Kristo atakapokuja kuitekeleza ghadhabu ya Mungu duniani, biblia inatuambia, kwa maangamizi yatakayotokea, damu itakayomwagika itakuwa ni nyingi sana, kiasi cha kufikia urefu wa  hatamu ya farasi, (ambayo hiyo ni sawa na futi 5 au 6 karibia kimo cha mwanadamu wa kawaida)..Na itaenda kwa umbali  wa maili 200 ambayo ni sawa na km 321. Hilo ni ziwa la damu.

Ufunuo 14:19 “Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.

14:20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili”.

Haijalishi itakuwa ni lugha ya picha au halisi, lakini hiyo inatupa kujua hali halisi jinsi kutakavyokuwa huku duniani wakati huo kwa wale watakaobaki, wanadamu wataadimika kama dhahabu..

Hivyo sisi hatupaswi kuchukulia, kirahisi rahisi haya maisha, ni kujihakiki je! Tupo ndani ya wokovu au la, kama hatupo basi, huu ndio wakati wa kuyatengeneza mambo yetu sawa, kwasababu kipindi hicho hakipo mbali.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.

UFUNUO: Mlango wa 16.

YEZEBELI ALIKUWA NANI

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/12/16/tofauti-kati-ya-lijamu-na-hatamu-ni-ipi-kibiblia/