Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)

by Admin | 22 March 2022 08:46 am03

SWALI: Tunasoma yule mkushi alikuwa ni mwenye mamlaka chini ya Kandake Malkia wa Kushi.. Naomba kufahamu Neno Kandake lina maana gani?


JIBU: Filipo, Mhubiri wa injili, aliagizwa na Malaika wa Bwana, aende njia ya jangwani (Gaza), Lakini alipokuwa njia kushuka huko alikutana na huyu mkushi ambaye alikuwa ni towashi, ndipo akamuhubiria injili, na siku hiyo hiyo akabatizwa, baada ya hapo Filipo akatoweshwa na Roho Mtakatifu na kupelekwa  sehemu nyingine.

Matendo 8:26 “Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27  Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu”

Lakini biblia inasema huyu mkushi alikuwa ni mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi.  Kandake ni jina la Mamalkia wote wa nchi ya Kushi (Kushi ndio nchi ya Ethiopia). Kumbuka sio jina la mtu binafsi bali ni jina la cheo. Kama vile ilivyokuwa kwa Farao, au Kaisari. Kwamba wafalme wote waliitwa Farao, au Kaisari. Ndivyo ilivyokuwa kwa mamalkia wote wa Kushi waliitwa Kandake.

Ndio huyu towashi aliwekwa chini ya umalkia huo ili kuilinda na kuitunza hazina yote ya taifa hilo la Kushi. Na unaweza kujiuliza ni kwanini awe ni towashi?. Ilikuwa ni desturi, kwa falme nyingi za zamani, pindi wanapotaka kuwaweka chini ya mamalkia wao, na chini ya sekta nyeti kama hizo za fedha. Waliwaasi, watumwa hao, ili kusudi kwamba wasivutwe na tamaa za mwili, na pia wasifikirie kuacha utumwa wao, na kujali familia zao( yaani Watoto wao na wake), Zaidi ya maslahi ya nchi. Hivyo hiyo ilikuwa inawafanya wawe wanyenyekevu na wawe makini sana katika kazi walizowekewa chini yao.

Inatufundisha nini?

Hata kuwekwa chini ya kazi maalumu za Mungu ni hivyo hivyo, Kunategemea sana uaminifu wetu. Rohoni tunapaswa tuwe kama matowashi. Tufe kwa Habari za tamaa za ulimwengu. Kiasi kwamba hata ukijaribiwa kwa mali, hali yako ni ile ile, ukijaribiwa kwa uzinzi, hutikisiki, ukijaribiwa kwa umaarufu, unabakia kuwa yule yule, kama Bwana Yesu, hugeuki kuwa nabii wa uongo.

Hapo ndipo Bwana anapopahitaji sote tupafikie, ili atuamini na kutuweka katika kazi zake maalumu. Hivyo Bwana anataka tufanane na matowashi rohoni mwetu. Kama alivyokuwa Ayubu mtumishi wake (Ayubu 31:1, 25)

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

“Vya Kaisari mpeni kaisari”  ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?

Deraya ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 59:17

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Nini kinatokea baada ya kifo

GOGU NA MAGOGU, Katika biblia ni nani?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/03/22/nini-maana-ya-kandake-matendo-827/