Easter ni nini?..Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

by Admin | 14 April 2022 08:46 am04

Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

Jibu: Pasaka ni sikukuu ya kiyahudi, ambayo ilianza kuadhimishwa kipindi wana wa Israeli wanatoka nchi ya Misri, wakati ambao Mungu aliwaambia wapake damu ya mwanakondoo katika miimo ya nyumba zao ili Yule Malaika atakapopita asiweze kuwadhuru wazaliwa wao wa kwanza, Hivyo Yule malaika alipopita na kuikuta ile damu ya mwanakondoo katika miimo ya nyumba zao, alipita juu, (maana yake hakuingia katika hiyo nyumba kuua wazawaliwa wa kwanza).

Sasa kitendo hicho cha Malaika kupita juu, ndicho kinachoitwa Pasaka, (kwa lugha kiingereza “passover”). Kwa maelezo marefu kuhusu pasaka na umuhimu wake, na kama inaruhusiwa kusheherekewa mpaka sasa na sisi wakristo, fungua hapa >>PASAKA IPO KIBIBLIA?

Lakini swali lingine ni kuhusu Easter? Je Easter ni nini?, je ipo kwenye biblia? na je sisi wakristo tunaruhusiwa kuiadhimisha easter?.

Jibu: Neno Easter, halipatikani mahali popote katika biblia, kama jinsi pasaka linavyopatikana katika sehemu nyingi, katika biblia (Easter lenyewe halipo kabisa).

Sasa Easter kama haipo imetoka wapi katika Ukristo?

Asili ya Easter, ni mungu wa kipagani (wa kike), aliyeaminika kuleta “uzao” kama vile “baali”  alivyokuwa.. mungu huyu aliabudiwa na jamii za watu wa Saxons, ambao kwasasa ni maeneo ya Ujerumani, na aliitwa “easter” kutokana na “mawio ya jua”. Upande jua linapochomoza, uliaminika kuwa ni upande wa neema na ndio unaomstahili huyu mungu mke, hivyo upande wa mashariki ni “East” kwa lugha ya kiingereza, kwahiyo kwa heshima ya mungu huyo wa uzao ndio wakamwita “easter”..yaani “wa mashariki”.

Na mungu huyu “easter” alikuwa anatolewa sadaka za kafara kipindi kile kile cha sikukuu za pasaka za kiyahudi, tarehe hizo zilikuwa zinagongana, kipindi ambacho Wayahudi wanasheherekea pasaka, ndio kipindi ambacho watu hao wa-Saxons na wengine wengi walikwenda kumtolea mungu wao huyo easter sadaka.

Kwasababu ni kawaida ya shetani kutafuta kuchanganya ukristo na upagani, alinyanyua watu kadhaa na kuoanisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu, na siku ya sadaka za mungu huyo “easter”. Hivyo ili desturi na kumbukumbu la mungu wao huyo “easter” lisife kabisa kabisa, ndipo wakaiita ile jumapili ya kufufuka kwa Bwana kama “jumapili ya easter”.

Sasa swali ni je! Na sisi wakristo tunaruhusiwa kuadhimisha easter kama sherehe ya kufufuka kwa Bwana Yesu?

Siku ya kufufuka Bwana Yesu, itabaki pale pale, na ni vizuri kuiadhimisha, kwasababu ni siku ya ushindi wetu, siku ya matumaini, na siku ya Shangwe, Mitume na watakatifu wote, kipindi wamejifungia ndani kwa hofu ya wayahudi, siku walipomwona Bwana kafufuka walifurahi furaha kuu.

Luka 24:34 “wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.

35 Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate.

36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.

37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.

38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.

41 BASI WALIPOKUWA HAWAJAAMINI KWA FURAHA, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?”.

Hivyo na sisi hatuna budi kuiadhimisha siku hiyo  kwa furaha nyingi, katika siku ile ile Bwana aliyofufuka, (yaani Jumapili ya pasaka), haijalishi watu wanaiitaje hiyo siku, watu wameipa jina gani, hata kama wangekuwa wameipa jina la “siku kumwabudu shetani” sisi hatutazami majina watu walioyapa siku, (tunaitazama siku yenyewe).. hata siku tulizozaliwa tukizifuatilia katika historia tutakuta zimepewa majina ya ajabu ajabu, lakini wau hawaachi kuziazimisha kisa tu zimepewa majina ya ajabu, au zimeangukia katika tarehe za kuadhimisha mambo mabaya..

Leo ukifuatilia katika historia au kumbukumbu, utakuta kila tarehe imengukia katika maandimisho fulani ya sikukuu za kipagani, hivyo hatuwezi kuacha kufanya mambo ya msingi katika hizo siku, na kuzifuata kalenda za kipagani.

Kwahiyo sisi wakristo tunasheherekea siku ya kufufuka kwa Bwana kama “jumapili ya ushindi” na si kama “easter”. Na hatusheherekei kipagani.

Siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu, tunapoiadhimisha kwa kwenda Bar, kulewa hapo tumeisheherekea easter, na si siku ya kufufuka kwa Bwana, siku ya jumapili ya kufufuka kwa Bwana tunapoisheherekea kwa kwenda disko, au kwenye kumbi za anasa, hapo tutakuwa tunamwadhimisha mungu “easter” na si “ufufuo wa Bwana”. Kwasababu waliokuwa wanamwadhimisha huyo mungu mke easter, katika siku hiyo walikuwa wanalewa na kucheza kipagani na kumtolea sadaka.

Lakini sisi wakristo hatuadhimishi/kusheherekea siku hiyo kipagani hivyo, bali siku ya kufufuka kwa Bwana ni siku ya kufanya ibada, ni siku ya kutafakari maisha yetu ya ukristo, tangu tumempokea Yesu mpaka sasa tumeshapiga hatua kiasi gani?..na kama tumerudi nyuma basi tutengeneze mambo yetu, ni wakati wa kutafakari ni mambo yako mangapi mazuri ya kiroho, yaliyokuwa yamekufa, na je yamefufuka!.. Kama bado ni wakati wa kutafuta kuyafufua.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

 Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

SHUSHANI NGOMENI NI WAPI KWA SASA?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/04/14/easter-ni-nini-na-je-tunaruhusiwa-kuisheherekea/