Kusemethi ni nini katika biblia?

by Admin | 16 April 2022 08:46 pm04

Kusemethi au kusemethu ni nafaka inayokaribia kufanana sana na Ngano kimwonekano na kiladha. Nafaka hii ni familia moja na nafaka ya Ngano.

Miaka ya zamani kabla ya Kristo, nafaka ya Kusemethi ndiyo iliyokuwa inatumika kama nafaka kuu ya kutengenezea mikate, Zaidi hata ya Ngano, lakini baada ya Kristo, Nafaka ya Ngano, ilianza kukubalika Zaidi duniani kote na kupata nguvu duniani kuliko Kusemethi. Kiasi kwamba mpaka kufikia leo hii ukitaja nafaka ya Kusemethi hakuna hata mtu anayeijua.

Ngano leo imepata nguvu kuliko Kusemethi, kama vile mafuta ya Alizeti, yalivyo na nguvu kuliko mafuta ya Mawese. Lakini Pamoja na hayo bado yapo maeneo machache ya dunia (Sehemu za Ulaya), wanalima Kusemethi na kuitumia kutengenezea mikate na vyakula vingine.

Katika biblia tunaona nafaka hii ikitajwa mara kadhaa, sehemu ya kwanza tunaona ikitajwa kipindi wana wa Israeli, wanaondolewa Misri na Bwana.

Kutoka 9:29 “Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia Bwana mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya Bwana.

30 Lakini, wewe na watumishi wako, najua ya kuwa ninyi hamtamcha Bwana Mungu bado.

31 Kitani na shayiri zilipigwa; maana shayiri zilikuwa na masuke na kitani zilikuwa katika kutoa maua.

32 Lakini ngano na KUSEMETHU hazikupigwa; maana, zilikuwa hazijakua bado”

Vile vile tunaona ikitajwa katika kitabu cha Ezekieli.

Ezekieli 4:9 “Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na KUSEMETHI, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula”.

Unaweza kusoma pia Isaya 28:23, utaona nafaka hiyo ikitajwa..

Kama kuna baadhi ya Mazao na vyakula vilivyokuwa vinakubalika zamani za kale, lakini leo hii vinaonekana havina thamani yoyote..vile vile vitu vingine vyote siku moja vitapita na kuwa si kitu, lakini wamtumainio Bwana watadumu milele.

1Yohana 2:17 “Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, BALI YEYE AFANYAYE MAPENZI YA MUNGU ADUMU HATA MILELE”.

Zaburi 125:1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, NDIVYO BWANA ANAVYOWAZUNGUKA WATU WAKE, TANGU SASA NA HATA MILELE”.

Je na wewe unamtumainia Bwana? Au ulimwengu?..

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka!.(Kumbukumbu 25:4)

Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?

Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/04/16/kusemethi-ni-nini-katika-biblia/