Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Masuke ni nini  katika biblia?

Masuke ni ile sehemu ya nafaka inayotoa ua na mbegu ndani yake, Kwamfano Ngano suke lake linachipuka kwa pale juu, tazama picha, na nafaka kama mahindi suke lake ndio lile linalochipukia hindi lenyewe. Lakini nafaka yote sio suke, wala hindi lote sio suke, bali ile sehemu inayotoa mbegu au ua au tunda ndio inaitwa suke.

suke la ngano

suke la hindi

Hivyo  zamani, kama mtu akitaka kula ngano iliyo mbichi, ambayo kiafya ilikuwa haina shida, kwani jamii za watu wa mashariki ya kati kama vile wapalestina na waarab,  zamani na hata sasa, wanaoutarabu huo wa kula, nafaka mbichi, hususani ngano ambayo haijapikwa..

Na katika kula kule, ni sharti, uipukuse pukuse au uipure pure kwanza ili kuondoa yale makapi yake, ibakie tu ngano, kisha ndio uile.

Sasa zamani Mungu alishatoa maagizo, kuwa kama mtu ukisikia njaa, na akakutana na shamba la jirani pembeni yake, unayoruhusu ya kwenda na kula kile kilicho katika shamba lile, lakini sio kuvuna na kuondoka navyo.

Kumbukumbu 23:25 “Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako”.

Sasa utaona tukio lingine kuna wakati Bwana Yesu alikuwa anapita na wanafunzi wake, na wanafunzi wake walikuwa na njaa, na kwa bahati nzuri wakakutana na shamba la nafaka njiani, kama tunavyoijua habari wakaingia na kuanza kupura yale masuke ili wale ngano, na siku hiyo ilikuwa ni siku ya sabato.

Luka 6:1 “Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao”.

Na  mafarisayo walipoona  wakaanza kuwashutumu kuwa wanaihalifu sabato kwa wanachokifanya, ndipo Bwana Yesu akawaeleza habari ya alichofanya Daudi alipokuwa na njaa jinsi alivyokula ile mikate ya wonyesho ambayo sio sahihi yeye kuila bali makuhani tu peke yao.

Na mwisho kabisa  akawaambia mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.

Nasi pia Je ni sahihi kuingia katika shamba la mtu yeyote na kula matunda  ya mashamba yake, kwa mfano miwa yake, au machungwa yake bila ya kupewa ruhusu kwa kigezo cha mstari huo?

Tunapaswa tujue Israeli walipewa agizo hilo kama taifa, kwahiyo sheria hiyo ilijulikana kwa watu wote. Lakini sisi tuliokatika mataifa, tunaishi katikati ya makundi ya watu wengi, na asilimia kubwa sio wacha Mungu. Hivyo tunapaswa tutumie hekima, ya kwenda kuomba kwanza, vinginevyo ukikutana na mtu asiyekuwa na huruma ya kibinadamu anaweza kukuletea matatizo.

Bwana akubariki.

Hivi ni baadhi ya vifungu vingine vinavyolizungumzia Neno hilo  “Masuke”

Marko 4:28 “Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.

29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika”.

 

Mwanzo 41:5 “Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.

6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.”

Walawi 23:14 “Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote”.

Soma pia Mathayo 12:1  na Marko 2:23

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

HERODE NA PILATO, MAADUI WAWILI WAPATANA.

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments