Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

Bisi ni nini?


Kama wengi tunavyofahamu bisi kwa mazingira yetu ni yale mahindi yanayokaangwa na kufutuka na pale yanapobadilika na kuwa na mwonekano mwingine (mweupe mweupe ) huliwa. Kwa wengine wamezoea kuyaita Popcorn lugha ya kigheni. Tazama picha kushoto.

Lakini kwa wayahudi, na jamii nyingi za watu wa mashariki ya kati, bisi zao haziwi kama hizi zetu za mahindi bali zao zinakuwa za ngano, na zinakaangwa vile vile kama zinavyokaangwa za mahindi isipokuwa tu  mwonekano wake haubadilika sana, kama ulivyo  wa mahindi.

Kuona jinsi inavyoandaliwa na mwonekano wake, tazama video hii >>>

https://www.youtube.com/watch?v=5fSY4YCVSoM

bisi za nganoHivyo mahali popote unapokutana na neno hili Bisi kwenye biblia basi ujue ni hii inayotengenezwa kwa ngano, na sio mahindi.

Kwamfano ukisoma biblia, utaona, Mungu anawapa wana wa Israeli maagizo kuwa pindi watakapovuna mavuno yao ya kwanza, wasile kwanza chochote katika walichokivuna, ikiwemo bisi, au masuke, mpaka watakapoleta kwanza kile kinachomstahili Mungu.

Walawi 23:14 “Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote”.

Utalisoma Neno hilo tena katika vifungu hivi;

Ruthu 2:14 “Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza”.

1Samweli 17:17 “Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako;

18 ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao.

1Samweli 25:18 “Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

19 Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.

Yoshua 5:10 “Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.

11 Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo”.

Soma pia, 2Samweli 17:28,

Je! Tunapaswa tukumbuke nini, kila tunapolisoma hili Neno?

Ni kwamba hata sisi, kwa kila Mungu anachotubariki, tusifikirie kula kwanza, mpaka tutakapohakikisha fungu la Mungu tumelitenga na kulitoa. Biblia imetumia neno bisi,  kwasababu ni chakula chepesi sana kukipika, ni kitendo cha kuweka kwenye sufuria na kukikaanga na kula, jambo ambalo halihitaji maandalizi mengi kuandaa, tofauti na vyakula vingine vya ngano, hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza kuvuna shamba lake, na hapo hapo akaenda kuchukua ngano hiyo na kukaanga mara moja na kula. Lakini hata hivyo Mungu kakataza. .. Hivyo na sisi, hatupaswi kufikiria kutumia hata  kwa vocha au kwa chipsi kile Mungu anachotubariki, kabla hatujalitenga fungu lake pembeni.

Hivyo ndio Mungu atakavyotubariki.

Shalom.

Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.

 Pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Choyo ni nini kibiblia? (Luka 12:15, Zaburi 10:3)

USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments