Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Neno kuwiwa maana yake ni “kudaiwa”.  Mtu anaposema ninawiwa kiasi fulani cha fedha maana yake ni “anadaiwa kiasi fulani cha fedha”, Au mtu anaposema ninamuwia mtu fedha, maana yake ni “anamdai mtu kiasi fulani cha fedha”. Hivyo kuwiwa/kuwia ni neno la kiswahili cha zamani lenye maana ya kudai au kudaiwa.

Katika biblia tunaona mifano kadhaa ambapo neno hili lilitumika.

Mathayo 18: 22  “Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

23  Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

24  Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

25  Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni

26  Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

27  Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni”.

Mistari mingine katika biblia yenye neno hilo “kuwiwa” ndani yake ni Luka 16:7 na Warumi 13:8.

Mbali na hilo, Biblia inatufundisha kuwa baada ya kuokoka na sisi pia tunakuwa na deni la kwenda kuwapelekea wengine habari za wokovu. Hivyo tunakuwa TUNAWIWA na watu wa ulimwengu habari za wokovu.

Hivyo hatuna budi kuipeleka injili kwa wengine, ambao wapo nje ya wokovu, kwa karama zetu, kwa  mali zetu na kwa nguvu zetu, kwasababu hilo ni deni kwetu.

Kama Mtume Paulo alivyosema mahali fulani kwamba ANAWIWA na watu wa aina mbali mbali, katika kuwapelekea injili..

Warumi 1:13  “Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.

14  NAWİWA NA WAYUNANİ na wasio Wayunani, NAWİWA na wenye hekima na wasio na hekima.

15  Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.

16  Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Hivyo pia na sisi baada ya kuokoka ni wajibu wetu, kuipeleka injili kwa watu ambao hawajaokoka, roho zao ni deni kwetu, kwahiyo ni lazima kuwapelekea habari njema za wokovu pasipo kuionea haya injili, kwasababu injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu.

Marko 16: 15  “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16  Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.(Marko16:15.) Yesu Anamaanisha nini kusema MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

EPUKA KUTOA UDHURU.

BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu;?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments