Hirimu ni nini?
Hirimu ni mtu aliye katika kundi la umri wako (rika). Kwamfano tukisema, Petro na Yohana ni hirimu moja, tunamaanisha Petro na Yohana ni watu wa umri mmoja.
Lakini kibiblia hirimu linakwenda mbali kidogo zaidi ya hapo, mahali pengine linamaanisha kijana mdogo.
Kwamfano mistari hii inazungumzia hirimu kama mtu wa umri mmoja naye.
Danieli 1:10 “Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme”.
Hapo ni Yule mwangalizi wa Vijana, towashi akiwaeleza akini Danieli hofu yake juu kukunjamana sura zao, pale vijana wenzao wa rika lao watakapoitwa nyumbani kwa mfalme na kuonekana wananawiri kushinda wao, atauliwa yeye.
Soma tena..
Wagalatia 1:14 “Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. 15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,”
Wagalatia 1:14 “Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
15 Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,”
Hapo mtume Paulo anazungumzia jinsi alivyofanya bidii ya kuzishika dini za kiyahudi kuliko hata watu waliokuwa wa rika lake, au umri wake, vijana wenzake.
Lakini katika vifungu hivi, vinalitaja neno hili, vikimaanisha kijana mdogo.
Waamuzi 8:14 Ndipo akamshika mtu mmoja hirimu katika watu wa Sukothi, akamwuliza; naye akamwandikia majina ya hao wakuu wa Sukothi, na wazee wa mji, watu sabini na saba.
Soma pia..Waamuzi 17:7,11, 18:3
Hivyo, ni nini tunaweza kujifunza kutokana na Neno hili?
Hata sisi tupo katika marika, tujiulize katika marika tuliyopo, ni mambo gani ya maana tunafanya kwa Mungu etu. Upo katika rika la miaka 12 angalia kwenye biblia waliokuwa na miaka hiyo walikuwa na bidii gani kwa Mungu. Yesu alipokuwa na umri huo, alikuwa hekaluni akijifunza sheria ya Mungu, je na wewe unafanya hivyo?
Upo katika rika la miaka 30, jiulize katika umri huo, unatenda jambo gani katika ufalme wa mbinguni? Bwana Yesu alipokuwa katika umri huo, alianza kuitenda kazi ya Mungu kwa nguvu akijua kuwa muda wake aliobakiwa nao kuishi duniani ni mchache.. Je, na wewe uliye katika rika hilo unalijua? Hirimu yetu Kristo Yesu alitendaje katika umri huo?
Vivyo hivyo upo katika miaka 40, au 50, au 70 au 80 jiulize ni nini unakiingiza katika ufalme wa mbinguni, Je ni kutwa kuchwa kusumbukia ya ulimwengu? Je, ni elimu tu, Je ni familia tu, au ni nini?. Musa alikuwa na miaka 80 alipoanza kumtumikia Mungu lakini utumishi wake aliuthamini, kana kwamba alikuwa na miaka 20, Je! Na wewe unafanya hivyo?
Kumbuka biblia inasema..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.
Heshimu umri wako, tambua ni nini unapaswa ufanye kwa wakati huo.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Choyo ni nini kibiblia? (Luka 12:15, Zaburi 10:3)
Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?
Baadhi ya watu na misemo ambayo haipo katika biblia.
IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.
UNYAKUO.
Rudi Nyumbani:
Print this post