Baadhi ya watu  na misemo ambayo haipo katika biblia.

Baadhi ya watu  na misemo ambayo haipo katika biblia.

Ifuatayo ni baadhi ya misemo, ambayo ipo katika jamii yetu, ambayo inadhaniwa kuwa ipo kwenye biblia lakini kiuhalisia haipo kabisa, aidha imetungwa na watu tu au inapatikana kwenye vitabu vingine tofauti na biblia.

  1. Jisaidie nami nitakusaidia

Huu msemo haupo kabisa kwenye biblia takatifu, ingawa umekuwa ukitumika na hata wakristo wakiamini kuwa kuna mahali kwenye biblia Mungu alisema “jisaidie nami nitakusaidia”. Hivyo kama mkristo badala ya kuutumia huo msemo ni afadhali ukatumika huu  “….. imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake (Yakobo 2:17 )”.

  1. Mungu si Athumani.

Huu pia ni msemo wa methali za kiswahili, ambao ni umekuwa ukitumika na hata wakristo baadhi wakiamini ni aya fulani katika biblia, una huo msemo.. Lakini katika biblia nzima huo mstari haupo. Hivyo badala ya kuutumia huo ni afadhali ukatumika huu “Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?( Hesabu 23:19)”.

  1. Mungu hamtupi Mja wake.

Huu usemi pia haupo kwenye biblia takatifu, ingawa hauna tafsiri mbaya, lakini haupo kwenye maandiko… Hivyo badala ya kuutumia huo ni vizuri, ukajizoeza kuutumia huu ambao upo kwenye maandiko… “Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake Maombolezo 3: 31”

  1. Mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye.

Msemo huu sio tu haupo kwenye biblia, lakini ni msemo wa uliotengenezwa na adui shetani asilimia mia..kwasababu ni kinyume cha maneno ya Bwana Yesu mwenyewe aliyoyasema katika..

Mathayo 5:43  “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44  lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.

          5. Kila Nafsi itaonja mauti:

Huu ni msemo maarufu sana, lakini haupo kabisa kwenye biblia..Na zaidi ya yote ni kinyume cha Biblia. Kwasababu biblia ambalo ndio Neno la Mungu inasema.. watakuwepo watu ambao unyakuo utawakuta wakiwa hai, na hawa watakuwa miongoni mwa watu ambao hawataonja mauti kabisa.. Hivyo sio wote watakufa..

1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”

Yafuatayo ni majina ambayo hayapo katika katika biblia.

  1. Mohamed

Jina hili halipo kabisa kwenye biblia, wala hakuna mtu mwenye jina kama hili katika biblia nzima. Yapo majina kama Yohana, Yuda, Anania ambayo yameonekana katika biblia sehemu mbali mbali, kwa watu tofauti tofauti, yakijirudia lakini jina hili Mohamedi  halipo hata kwa mtu mmoja katika biblia nzima, aidha kwa watu wa Mataifa au katikati ya wana wa Israeli. Hivyo hadithi zozote zinazotaja uwepo wa mtu mwenye jina hili katika biblia ni hadithi za kutunga na zenye maudhui ya kupotosha.

  1. Israeli Mtoa roho

 Usemi huu ni maarufu, ukimlenga malaika yule anayehusika na kutoa roho za watu, yaani mtu anapokaribia kufa kuna malaika anakuja, almaarufu kama “Israeli Mtoa roho” ndiye anayehusika katika kuiondoa roho ya mtu. Usemi huu, na jina hilo, halipo kabisa katika biblia nzima, hivyo ni usemi uliotungwa na watu.

Yapo na mambo mengine mengi, ambayo yanaaminika na wengi kuwa yapo katika ndani ya Biblia lakini kiuhalisia hayapo. Hivyo ni wajibu wetu kuwa makini, na kujifunza kuyasoma maandiko wenyewe kuliko kusubiria tu kusimuliwa au kuhadithiwa, kwasababau adui yetu shetani hajalala usingizi, usiku na mchana anatunga mbinu mpya za kuweza kututoa katika mstari, na kuyageuza maandiko, hivyo tuwe macho.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Wapunga Pepo wanaozungumziwa kwenye biblia ni watu wa namna gani?

Katika Yakobo 1:13 Biblia inasema Mungu hamjaribu mtu, lakini tukirudi kwenye kitabu cha Mwanzo 22:1 tunaona Mungu alimjaribu Ibrahimu. Hapo naomba mwanga zaidi.

Je ni sahihi kumtenga mtu anapofanya dhambi kanisani?

Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments