Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?

by Admin | 18 April 2022 08:46 am04

Kukana ni kitendo cha kumkataa mtu aliyekaribu nawe, kwa hofu/shinikizo Fulani pengine aidha kwa hofu ya kuaibishwa, au kudharauliwa, au kuuliwa au kutengwa, au kuchekwa n.k. Lakini kimsingi sio kwamba humpendi au huyo mtu hana thamani yoyote kwako.

Lakini kusaliti, ni jambo  baya Zaidi, kwasababu linahusisha, kumkataa mtu Fulani aliye karibu nawe kwa hiari yako mwenyewe, pasipo shinikizo lolote, kwa maslahi yako binafsi, ni kitendo cha moyo-baridi kabisa.

Kwamfano Petro alimkana Bwana, kutokana na shinikizo la hofu ya yeye kukamatwa na kwenda kupigwa kama Bwana..Lakini hapo nyuma utaona, alidhubutu kumuhakikisha kabisa Bwana kwamba hata wenzake wote wajapomkana, yeye hatofanya hivyo (Mathayo 26:33-35)

Utaona tena hata baadaya ya kutubu kwake baadaye, alipokutana na Bwana kule baharini bado alimuhakikisha mara tatu kuwa anampenda yeye..(Yohana 21:15-17). Kuonyesha kuwa ni shinikizo ndio lililompeleka kufanya vile, lakini moyo wake bado upo kwa Yesu.

Lakini Yuda tangu mwanzo alikuwa hampendi Bwana, japokuwa yeye alipendwa sana, mahali pengine mpaka Yesu akawa anampa siri zake za ndani japokuwa alikuwa mwizi, biblia inasema hivyo katika Zaburi 41:9

9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.

Lakini kinyume chake akarudisha mabaya badala ya mema. Utaona yeye mwenyewe kwa hiari yake akawafuata wakuu wa makuhani bila shinikizo lolote, akawaambia mtanipa nini, nikiwapa Kristo!. Wakamuahidia Pesa. (Mathayo 26.14-16)

Usaliti unafanana na mtu ambaye yupo tayari kumuua au kumletea madhara mzazi wake, kwa faida zake mwenyewe, pengine mali, au cheo, au heshima. Bila kujali kuwa yeye ndiye aliyemnyonyesha, aliyemtunza tangu akiwa tumboni, ndiye aliyemsomesha na kumvisha n.k.

Lakini kibiblia, vyote viwili yaani “kukana na kusaliti” hatupaswi kuwa navyo kwa Bwana wetu.

Leo hii wapo watu wanaomsaliti Bwana..Ndio hawa manabii na makristo wa uongo. Ambao wanajua kabisa waliokolewa kwa thamani, walitolewa chini matopeni, lakini wanapokuzwa kidogo, wanaanza kumgeuza Kristo kuwa biashara yao. Wanaacha utumishi walioitiwa, wanatumia fursa ya Kristo, kuyashibisha matumbo yao tu… Hawa ndio wakina Yuda.

Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.

Lakini Wakanaji, ni wakristo wote, ambao mioyo yao haipo kikamilifu kwa Bwana..wapo nusu nusu, ndio wale wakipitia dhiki kidogo, wapo tayari kumwacha Kristo, kisa ndugu, au wazazi, au shughuli, au ujana au anasa..hali na mazingira yanawafanya wamkane Bwana wao moja kwa moja, kwa matendo yao.

Na hii ni mbaya sana Bwana Yesu mwenyewe alisema..

Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Umeona?..Lipi bora, uchukiwe na ulimwengu leo, lakini siku ile utukuzwe na Yesu, au leo hii umkane halafu siku ile ukwane naye? Majibu yanajulikana.

Hatupaswi kuogopa kuonekana washamba kisa tumeokoka, hatupaswi kuogopa kupigwa, au kuchekwa, au kuonekana tumerukwa na akili sababu ya Yesu, mwokozi wetu. Bali tumkiri yeye kwa matendo yetu, kwasababu hata yeye mwenyewe alidharauliwa lakini akayapuuzia maradhau yao (Isaya 53:3).

Hivyo sote tujifunze kujitwika misalaba yetu tumfuate Kristo. Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu,.

Bwana atubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti?

Chapa zake Yesu ni zipi hizo?

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

WAPENZI, MSIIAMINI KILA ROHO.

Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )

Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/04/18/kukana-na-kusaliti/