Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).

by Admin | 27 April 2022 08:46 am04

Ayubu 21:10 “Fahali wao HUVYAZA wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba”.

Kuvyaza ni lugha ya “kuzaliana” inayotumika kwa Wanyama wa kiume. Badala ya kusema “Ng’ombe dume anapanda”, lugha nzuri ni kusema “ng’ombe anavyaza” . Neno hili limeonekana mara moja tu katika biblia..

Ayubu aliiona njia ya wasio haki, kwamba  mali zao zinapongezeka, na mafahali yao YANAPOVYAZA na, na ng’ombe wao wa kike wanavyozaa kwa wingi, na huku wanamkataa Mungu.. mwisho wao utakuwa ni kushuka kuzimu kwa ghafla.

Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?

8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.

9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.

10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.

11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.

12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.

13 SIKU ZAO HUTUMIA KATIKA KUFANIKIWA, KISHA HUSHUKA KUZIMUNI GHAFULA.

14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako.

15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?”.

Vile vile Daudi naye aliliona hilo hilo, kuwa mafaniko ya Mtu mwovu, mwisho wake ni kuangamia.

Zaburi 92:7 “Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele”

Na Sulemani naye aliliona hilo na kwa uweza wa Roho akasema..

Mithali 1:32 “…kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.

Hii ikifunua kuwa mafanikio sio uthibitisho wa kwanza kwamba tumekubaliwa na Mungu, ukilima na kuvuna na huku moyoni umemwacha Mungu jua hayo mafaniko, yatakuangamiza..Ukifanya biashara na ukafanikiwa sana, sio uthibitisho wa kwanza kwamba njia zako ni sawa mbele za Mungu.. Zaidi sana Bwana Yesu alisema, itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu mzima, na kisha akapata hasara ya nafsi yake?.. kumbe inawezekana mtu akaupata hata ulimwengu mzima, lakini bado akapotea!. Hivyo mafanikio sio kitu cha kwanza cha kutafuta, bali tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake.

Na ufalme wake na haki yake ni kumwamini Yesu, na kutubu na kubatizwa na kuishi Maisha matakatifu.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

KUOTA UNA MIMBA.

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?

Maji ya Farakano ni nini katika biblia?

Nini maana ya usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka!.(Kumbukumbu 25:4)

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/04/27/kuvyaza-ni-nini-katika-biblia-ayubu-2110/