Nini tofauti ya Majira na Wakati?

by Admin | 14 November 2022 08:46 pm11

Wakati ni “kipindi cha Muda” kwa kusudi Fulani, Kwamfano ukipanga kesho saa 7 mchana uende sokoni kununua bidhaa.. sasa huo muda wa “Saa 7 mchana” ndio unaoitwa “wakati wa kwenda kununua bidhaa”

Lakini “Majira” ni kipindi cha Muda ambacho ni cha “Msimu” Kwamfano Msimu wa mvua za masika hayo ni “majira ya masika”..msimu wa matunda ya maembe “hayo ni majira ya maembe”.. Msimu wa baridi, unaitwa “Majira ya baridi”.. Msimu wa joto huo unaitwa “majira ya joto”.

Mwanzo 8:22 “Muda nchi idumupo, MAJIRA YA KUPANDA, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma”

Sulemani alizidi kuliweka hili vizuri kitabu cha Mhubiri..

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna MAJIRA YAKE, Na WAKATI kwa kila kusudi chini ya mbingu. 

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; 

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza”

Unaweza kusoma zaidi juu ya Majira na Nyakati katika Mwanzo 7:21, Zaburi 1:3, Walawi 15:25,  na Ayubu 39:1.

Lakini pia yapo majira na nyakati katika makusudi ya Mungu. Na kusudi kuu ambalo ni muhimu kulijua majira yake ya kurudi kwa BWANA YESU MARA YA PILI!.. Hatuwezi kujua “Wakati” lakini “majira” ya kurudi kwake, tunaweza kuyajua… Ni kama vile hatuwezi kujua siku au wakati mvua itanyesha, lakini tunajua msimu, kuwa tukishaufikia huo msimu basi tunajua  siku yoyote mvua itaanza kunyesha.

Vile vile Bwana Yesu hakutoa wakati wa kurudi kwake, lakini alitoa “MAJIRA” Kwamba tuyafikiapo hayo majira basi tutajua kuwa WAKATI wowote atatokea mawinguni.

Marko 13:32 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.

33  Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui WAKATI ule utakapokuwapo”

Sasa Majira ya kurudi kwake ni yapi, ambayo tukiyatazama tutajua kuwa yupo mlangoni?.

Si mengine zaidi ya yale tunayoyasoma katika Mathayo 24, Luka 21 na Marko 13... kwamba kutatokea “Tauni” mahali na mahali, kutasikika tetesi za vita mahali na mahali, kutatokea na magonjwa mfano wa Tauni mahali na mahali, vile vile kutatokea na manabii wengi wa uongo ambao watawadanganya wengi na upendo wa wengi utapoa na maasi yataongezeka.

Hivyo tukishaona hizo dalili basi tunajua kuwa tayari tumeingia katika MAJIRA YA KURUDI KWAKE…na kwamba wakati wowote atatokea mawinguni, na hivyo tunapaswa tuchukue tahadhari… Na majira yenyewe ndio haya tuliyopo mimi na wewe..

Ndugu yangu Yesu anarudi wakati wowote!!, na yeye mwenyewe alituonya tuwe macho!, tukeshe katika roho kila siku, ili siku ile isije ikatujia ghafla..

Lakini tukifumba macho yetu na kukataa kuyatazama haya majira na kuchukua tahadhari.. basi tutaangukia katika like kundi la wanafiki Bwana Yesu alilolitaja katika Luka 12:54-56 na siku ile itatujia ghafla na hatutapona.

Luka 12:54  “Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.

55  Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

56  Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, BASI, KUWA HAMJUI KUTAMBUA MAJIRA HAYA?”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

WAKATI ULIOKUBALIKA NALIKUSIKIA

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.

KUOTA UNAENDESHA GARI.

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/11/14/nini-tofauti-ya-majira-na-wakati/