INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.

by Admin | 18 November 2022 08:46 am11

Tukiijua nguvu Mungu aliyoiweka katika injili, basi tutakwenda kuihubiri kwa bidii zote.

Wengi wetu tunasubiri tufikie kimo Fulani cha maarifa ndipo tukahubiri, wengine tunasubiri tupate upako Fulani au uweza Fulani ushukao juu ndipo tukahubiri.. wengine tunangoja unabii na maono au sauti utuambie tukahubiri ndipo tukaianze kazi hiyo… Wengine tunasubiri tupitia kwanza madarasa fulani ya theolojia ndipo tukaitangaze habari njema.. Kuanzia leo anza kufikiri tofauti!..

Hebu tusome maandiko yafuatayo…

Warumi 1:15  “Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.

16  Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Hapo mstari wa 16, maandiko yanasema “INJILI NI UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU”.. Kumbe injili ni “UWEZA” yaani nguvu au maajabu… na Zaidi sana si wa mwanadamu bali wa Mungu. Ikiwa na maana kuwa NGUVU ILIYOPO KATIKA INJILI, inatoka kwa Mungu..na wala si kwetu!.

Tukilijua hili tutapata ujasiri wa kwenda kuhubiri bila hofu, bila mashaka yoyote… bila woga wowote, kwasababu katika kuhubiri ndipo Mungu atashughulika katika kuuingiza wokovu katika watu, na wala si kazi yangu mimi kuwageuza watu!.. kwasababu Injili yake NI UWEZA WAKE, ambao unaleta wokovu ndani ya mtu.

Ndugu baada ya kumwamini Bwana Yesu kama Mwokozi wa maisha yako, na kutubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi na kubatizwa fahamu kuwa tayari umekidhi vigezo vya kwenda kuwahubiria wengine habari njema… usingoje ufikie ukamilifu Fulani!.. usingoje uanze kunena kwa lugha, usingoje uanze kuona maono!.. wewe nenda kahubiri hayo ambayo tayari umeshayajua.. na utaona uweza wa Mungu kwa hicho utakachokwenda kukihubiri.. utaona Mungu akiwaokoa watu na kuwafungua katika hicho hicho kidogo ulichonacho, kwasababu Injili ni UWEZA WA MUNGU!, na si uweza wa mwanadamu!.

Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hili kimaandiko.

Rejea wakati Bwana Yesu anawatuma wanafunzi wake wawili wawili kwenda kuhubiri, utagundua kuwa Bwana Yesu alianza kuwatuma wanafunzi wake hata kabla ya Pentekoste…na waliporudi walirudi kwa kushangilia jinsi watu walivyokuwa wakifunguliwa…

Petro alianza kuhubiri hata kabla ya kupokea Roho Mtakatifu, wewe leo unasubiri nini?.. Petro na mitume wote wa Bwana Yesu waalianza kuwaeleza watu habari toba na msamaha wa dhambi hata kabla ya kunena kwa lugha!, je wewe uliyemwamini Yesu leo unasubiri nini?.

Luka 10:17  “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako”

Hicho kidogo ulichonacho kinaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ndani ya watu, endapo ukiamua! Kwasababu injili NI UWEZA WA MUNGU wa kuwaokoa watu na si uweza wako wewe au mwanadamu mwingine yoyote.

Amka hapo ofisini kwako, anza kuhubiri habari za Yesu, usijiangalie kama unaweza kuongea au la!.. wewe hubiri Bwana atakuwa na wewe katika kuzungumza…kwasababu kuna UWEZA wa kiMungu katika maneno ya injili.. Wakati unahubiri watu hawataangalia kasoro zako bali watalisikiliza lile Neno la litawageuza.. na baada ya pale utashangaa jinsi Bwana anavyofanya kazi.

Bwana akubariki.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

JE! HAMPOTEI KWA SABABU HII?

USIMPE NGUVU SHETANI.

Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/11/18/injili-ni-uweza-wa-mungu-uuletao-wokovu/