Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.

by Admin | 18 December 2022 08:46 pm12

SWALI: Naomba kufahamu vifungu hivi tunavyovisoma katika Isaya 24:18-20 vinamaana gani?

Isaya 24:18 “Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.  19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.  20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.”

JIBU: Mstari hiyo inatupa picha ya dunia ilivyosasa katika hali ya roho. Imefananishwa na mlevi ambaye amelewa sana, na hivyo hawezi kujimudu tena.

Kama tunavyofahamu, mlevi kabla ya kudondoka mtaroni na kulala hapo hapo, huwa unayumba yumba sana, anapepesuka sana, hatua moja mbele, kumi nyuma, kwenda kulia, kwenda kushoto, hiyo yote ni anatafuta uwiano lakini anaukosa kwasababu kichwa chote kimeshatiwa uzito, kila kitu kilichombele yake anakiona kama kimeguzwa juu chini..

Hivyo kutembea kwake, hakuhusishi tena ubongo, bali uzoefu, na hatari zaidi pale atakapo jikwaa tu kidogo na kuanguka, basi safari yake inakuwa imeishia hapo, hawezi tena kunyanyuka, mpaka atakapolevu asubuhi.

Ndivyo dunia, ilivyo rohoni, nyakati hizi tulizopo, imelevywa sana kwa dhambi za wanadamu, na hivyo imepoteza muhimili wake, tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo, hatushangai sikuhizi kuona, majangwa mengi, ukame uliopitiliza, matetemeko makubwa ya ajabu, magonjwa ya kutisha kama Korona, Ebola kuzuka, mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo. Sasa haya yote hayajajizukia hivi hivi tu, bali ni kuleweshwa kwa dunia kwa dhambi zinazoendelea kuwa nyingi.

Ndugu yangu, tupo katika hatari kubwa; Hatari ya “hofu, mashimo, na mitego”, kama hayo maandiko yanavyosema, Ikiwa na maana kama tupo nje ya Kristo tujiandae, kukutana na mambo haya katika maisha yetu. Mtu ambaye hajaokoka, ni kwa neema za Mungu tu anaishi hadi sasa kwenye dunia hii inayowaya-waya kama machela.

Lakini kama tumeokolewa Bwana ameahidi kutuepusha nayo. Kwasababu unyakuo wa kanisa upo karibuni sana kutokea. Na baada ya hapo, ndipo huu ulimwengu utaanguka kabisa..

Ufunuo 6:12  “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13  na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.

14  Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15  Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16  wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17  Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.

Je! Unasubiri nini, usimkaribishe maishani mwako? Je! Unauhakika wa kesho? Vipi ikiwa utakufa leo, au Kristo amerudi ghafla sasa hivi utasema nini rafiki.. Kumbuka mipango yote ya mpinga-Kristo ipo tayari, injili imeshahubiriwa duniani kote, dakika tulizonazo ni za nyongeza tu, wakati wowote, parapanda italia, na hali halisi ilivyo tusidhani tuna miaka mingi mbele, muda umeisha kwelikweli, usipumbazwe na mambo ya ulimwengu ukadhani, Yesu harudi hivi karibuni. Ni kwasababu husomi biblia ndio maana unadhani hivyo. Injili ya sasa sio ya kubembelezwa tena, ni mtu mwenyewe kuona na kugeuka, na kuyasalimisha maisha yako. Sio wakati wa kutanga tanga, na maisha bali ni kumtafuta Mungu.

Bwana atusaidie.

Maranatha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UNYAKUO.

MFALME ANAKUJA.

TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?

TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/12/18/dunia-inalewa-lewa-kama-mlevi-nayo-inawaya-waya-kama-machela/