Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?

Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?

Jibu: Tusome,

Mathayo 11:19 “Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake”.

Kabla ya kujua kama Bwana Yesu alikuwa ni mlevi au la!..tujiulize kwanza kama alikuwa kweli Mlafi?.

Kama Bwana hakuwa mlafi basi ni wazi kuwa pia hakuwa mlevi.

Lakini swali la kujiuliza ni kwanini walimwona kama mlafi na Mlevi?

Jibu ni kwasababu muda mwingi alikuwa anashinda na wenye dhambi akiwafundisha.

Kikawaida ukionekana mara kwa mara unazungumza na walevi, au unashinda na walevi, ni rahisi na wewe kuzushiwa ni Mlevi hata kama si mlevi, vile vile unapoonekana mara kwa mara unaingia kwenye nyumba za watu, na wakati mwingine kula nao ni rahisi kuzushiwa ni mlafi.

Sasa Bwana Yesu naye alikuwa ni mtu wa kuzunguka mara nyingi kwenye nyumba za watu, hususani wenye dhambi pale walipomwalika, hivyo hiyo ikamfanya wale wasiomwelewa kufikiri ni mlafi, kufikiri kwamba anazunguka kwenye hizo nyumba kutafuta kula, kumbe Bwana hakuwa anaingia kwenye nyumba za watu kutafuta chakula bali kutafuta roho zao.

Utalithibitisha hilo siku alipokwenda kwa Zakayo mtoza ushuru katika Luka 19:2-8, na alipokwenda kwa Simoni mkoma katika Mathayo 26: 6-13, Na sehemu nyingine zote.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Bwana hakuwa mlevi, kama vile jinsi ambavyo hakuwa mlafi.. Ila alionekana na baadhi ya watu kama mlevi kutokana na jinsi alivyokaa muda mwingi na wenye dhambi, ambao ndani yake wamo walevi…

Lakini hekima yake ilikuwa na nguvu kuliko yao, kwasababu aliwaambia maneno yafuatayo..

Marko 2:16 “Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”.

Na sisi hatuna budi, kuiiga hekima ya Bwana Yesu, ya kuwapelekea injili wale wasio na afya, watu walio katika vifungo vya giza walio katika manyumba, walio katika masoko yao ya kujiuza miili yao, walio mahospitalini, mitaani n.k na sio muda wote kudumu kanisani tu!..mahali ambapo tayati kuna nuru, tayari kuna watu wenye afya.

Bwana atusaidie.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

JE! ULEVI NI DHAMBI?.

Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments