Kuna tofauti gani kati ya  “Edeni” na “Adeni”?

by Admin | 5 January 2023 08:46 am01

Nini tofauti kati ya Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:8) na bustani ya Adeni (Ezekieli 28:13 na  Yoeli 2:3)

Jibu:Tusome

Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa EDENI, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.

Isaya 51:3 “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama BUSTANI YA EDENI, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba”. 

Hapa tunaona ikitajwa bustani ya “Edeni” lakini tukisoma mahali pengine tunaona ikitajwa bustani nyingine ya “Adeni”

Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya ADENI, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari”

Yoeli 2:3 “Moto unakula mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na BUSTANI YA ADENI mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao”.

Na pia katika Ezekieli 31:9, Ezekieli 31:16-18, na  Ezekieli 36:35 utaona ikitajwa Adeni na si Edeni, swali je kuna utofauti wowote?

 Jibu ni la! hakuna utofauti wowote iliyopo kati kati ya “Adeni” na “Edeni”, hayo ni maneno mawili yenye maana moja, sehemu moja biblia imetaja Edeni, sehemu nyingine Adeni lakini maana ni ile ile..Na maana ya neno Edeni au Adeni ni “paradiso ya raha”.

Mungu alipoiumba dunia, alimweka mwanadamu wa kwanza katika bustani ya Edeni, na alikusudia mahali pale pawe Paradiso yake ya milele. Dunia yote ilikuwa ni nzuri, lakini pale Edeni palikuwa ndio kitovu cha utukufu wa mwanadamu.

Lakini baada ya shetani kumdanganya Hawa, ndipo Uovu ukaingia na kusababisha mwanadamu kuondolewa katika bustani ile, na Mungu kuitowesha kabisa!

Lakini Bwana ameahidi kuumba Mbingu Mpya na Nchi mpya (Isaya 65:17), ambayo itakuja baada ya utawala wa miaka elfu kuisha hapa duniani. Katika mbingu mpya na nchi mpya, Bwana ametuandalia mambo mazuri kuliko yaliyokuwepo Edeni, maandiko yanasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Mungu kawaandalia wale wampendao..(1Wakorintho 2:9).

Lakini ahadi hiyo kulingana na Neno lake ni kwa wale waliomwamini Yesu Kristo na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake.

Je umempokea Yesu?..kama bado unasubiri nini?. Mwamini leo na ukabatizwe katika ubatizo na ujazwe Roho Mtakatifu kulingana na Matendo 2:38.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Bustani ya Edeni ipo nchi gani?

EDENI YA SHETANI:

Je! Ni kweli Yesu alirejesha kila kitu kama pale Edeni?

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

MIGAWANYO MINNE (4), YA HUDUMA YA YESU.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/01/05/kuna-tofauti-gani-kati-ya-edeni-na-adeni/