Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?

by Admin | 9 February 2023 08:46 am02

Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe dhambi zako kabisa kabisa. Lakini hutasikia, hisia Fulani, au badiliko Fulani la wakati huo huo, kwani fikra zako za dhambi za zale bado zitaendelea kuzunguka kwenye akili yako. Hivyo wengi wakishaona hivi wanadhani kuwa Mungu hawajawasamehe, na hivyo wanaendelea kubaki katika mashaka, au kurudia rudia kumlilia Mungu awasamehe.

Na hapa hapa shetani ndipo anapata nafasi ya kuwatesa, na kuwakandamiza, wengine wanajikuta kila siku wanaomba Toba Mungu nisikie unisamehe!, Mungu nisikie unisamehe!, kumbe tayari Mungu alishawasamehe tangu siku ile ya kwanza walipomaanisha kweli kweli kugeuka na kukataa kurudia dhambi zao.

Ndugu, fahamu hata kama wewe utakuwa na kumbukumbu la nyuma la dhambi zako, lakini kwa Mungu ni tofauti, yeye akisamehe anasahau kabisa.

Waebrania 8:12  “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”.

Unapokwenda mbele za Mungu, lazima uamini kwa moyo wako wote umeshasamehewa, vita vya kimawazo vinavyoanza kuja tangu huo wakati, huna budi kuvishinda, kwa kuvipinga, ukisikia moyoni mwako unaambiwa, aah! Wewe dhambi zako ni nyingi, ile dhambi ulishamkufuru Roho Mtakatifu, pinga, kataa sema mimi nimeshasamehewa kwa damu ya Yesu Kristo.

Kisha unavyozidi kufanya hivyo baada ya kipindi Fulani utaona amani ya Mungu imekuvaa.

Lakini pia ni lazima ukumbuke kuwa yapo mambo yanayochangia pia kusamehewa dhambi zetu, na yenyewe ni sisi kuwasamehe waliotukosea kama wapo.

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 6:14  “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15  Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.Hivyo uombapo msamaha zingatia kuwa moyo wako ni mweupe kwa wengine.

Bwana akubariki

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA KUTUBU

Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?

TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!

KIFAHAMU KIGEZO  CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.

KUONGOZWA SALA YA TOBA

Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/02/09/nitajuaje-kuwa-nimesamehewa-dhambi-zangu/