VUNJA AGANO LA MAUTI.

by Admin | 24 October 2023 08:46 pm10

Mtu anaingiaje agano na mauti?

“Agano” kwa jina lingine ni “Mkataba”

Mtu anapoingia mkataba na mtu mwingine ni sawa na kaingia agano na mtu huyo.

Sasa mwanadamu pia anaweza kuingia Agano na Mauti, Ndivyo biblia inavyotufundisha kuwa mtu anaweza kuingia agano na Mauti na kuingia katika mapatano na kuzimu.

Isaya 28:18 “Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo”.

Na kama mtu ameingia Agano na Mauti ni lazima mauti itakuwa na nguvu juu yake,itamwandama popote anapokwe nda na itampata..hivyo ni lazima hilo agano livunjwe ili mtu huyo abaki huru, na uzima utawale ndani yake,

Sasa kinachomwingiza mtu katika agano la Mauti ni nini?..je ni ndoto anazoziota?, Au ni wachawi?, Au wanadamu?..

Jibu: Si wanadamu, wala wachawi, wala ndoto mtu anazoota bali ni “dhambi ndani ya mtu”…Biblia inasema “Mshahara wa dhambi ni Mauti”.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Sasa hapo hasemi “matokeo ya dhambi ni mauti” bali “mshahara wa dhambi ni mauti”.

Maana yake mtu anayefanya dhambi ni sawa na mtu anayefanya kazi za kumpatia mshahara..Kwamba ni lazima atakuwa na mkataba wa kazi (yaani agano la kazi) ili apokee mshahara.

Halikadhalika na mtu anayefanya dhambi, anakuwa kwanza ameingia agano na hiyo dhaambi na ndipo anapokea mshahara wake baada ya kuitendea kazi, na mshahara wake ndio “Mauti”.

Kwahiyo kumbe Agano la Mauti ni “dhambi”..Ikiwa na maana kuwa mtu akiondoa dhambi katika maisha basi atakuwa amelivunja hilo agano la Mauti lililo ndani yake!.

Kumbe mtu anayeabudu sanamu tayari yupo katika agano na mauti, kumbe mtu anayezini tayari kashaingia agano/mkataba na mauti, Kumbe mtu anayeiba tayari yupo katika agano na mauti?, Na kwamba siku yeyote atakumbana na Mauti ya mwili na roho, na hatimaye kutupwa katika ziwa la moto ambako huko kuna mauti ya pili. (Ufunuo 20:14 na 21:8)

Sasa hili agano la Mauti tunalivunjaje?…je ni kwa kuwekewa mikono na watumishi?, Au kwa kunywa maji na mafuta yajulikanayo kuwa ya upako?, Au kwenda kukemea hayo maagano?

Jibu la swali hili hatulipati pengine popote isipokuwa kwenye biblia.

Matendo 2:38 “Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Umeona kanuni ya Kuondoa dhambi?…si kwa kupakwa mafuta, au kuwekewa mikono kichwani…bali ni kwa KUTUBU NA KUBATIZWA.

Unapotubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi basi unapokea msamaha na papo hapo na lile agano la Mauti linavunjika!..sawasawa na maandiko hayo ya Isaya 28:18,

Isaya 28:18 “Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo”.

Lakini kama hakuna toba halisi na ubatizo basi agano la mauti bado lipo palepale..halijavunjika! Haijalishi mtu huyo atawekewa mikono na watumishi wangapi, au ataombewa na watu wangapi, au anaabudu dhehebu kubwa kiasi gani..kama bado hataki kuacha dhambi, zinazotajwa katika Wagalatia 5:19…basi Mauti bado ipo pale pale.

Tubu leo na Agano la Mauti litabatilika juu yako, kile kifo ambacho ulikuwa umekiona kimekukaribia kitapelekwa mbali nawe.. Na hakikisha toba yako inaendana na matendo, kama umetubui wizi, au uzinzi, au uchawi au jambo lingine lolote hakikisha kuanzia siku hiyo hurusii tena hayo..(Unafanyika kiumbe kipya).

Bwana atusaidie.
Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Je Adamu na Hawa, walikuwa hawafanyi mema kabla ya kula tunda?

Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?

DHAMBI YA MAUTI

MSHAHARA WA DHAMBI

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/10/24/vunja-agano-na-mauti/