Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?

by Admin | 27 March 2024 08:46 am03

(Maswali yahusuyo pasaka)

Swali: Je kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka, kwamfano mwaka 2023 pasaka ilikuwa ni Aprili 13, lakini mwaka huu 2024 ni Marchi 31, na inategemewa kubadilika tena katika mwaka ujao na miaka yote inayokuja, kwanini iwe hivyo, wakati Krismasi ni tarehe ile ile 25 miaka yote?


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa pasaka ni moja ya sikukuu 7 za wayahudi, na inasheherekewa na wayahudi katika kila terehe 14 ya mwezi wao wa Kwanza, ambapo mwezi wao wa kwanza unaangukia katikati ya mwezi Machi na Aprili kwa kalenda tunayoitumia sisi.

Lakini kuhusiana na kwanini tarehe za pasaka zinabadilika kila mwaka kwa upande wa wakristo, ni kutokana na MWONEKANO WA MWEZI.

Mwezi unapozuka mzima (yaani angavu/full moon) basi jumapili inayofuata ndiyo inayosherekewa na wakristo wengi kama jumapili ya pasaka.

Kuna miaka ambapo “mwezi mwangavu” unawahi kuchomoza na kuna miaka unachelewa. Ikiwa na maana kuwa kama mwezi mwangavu  utaonekana jumatano basi jumapili inayofuata itakuwa jumapili ya pasaka, ambayo itakuwa ni baada ya siku nne,  Kwamfano kwa mwaka 2023 mwezi mwangavu ulionekana jumatano ya Tarehe 5 Aprili, hivyo jumapili iliyofuata ya tarehe 9 ndio ikawa jumapili ya pasaka.

Lakini kwa mwaka 2024, Mwezi mwangavu umewahi kuonekana, kwani umeonekana Jumatatu ya tarehe 25 Machi, hivyo jumapili inayofuata ya tarehe 31 Machi, ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.

Lakini pia kwa mwaka 2025, Mwezi mwangavu unatarajiwa kuonekana jumapili ya tarehe 13 Aprili, hivyo jumapili itakayofuata ya tarehe 20 Aprili ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.

Kwahiyo hiyo ndio sababu kwanini tarehe hizo zinabadilika badilika kila mwaka, (ni kutokana na mwonekano wa mwezi).

Sasa kujua pasaka ni nini na kama wakristo ni halali kuiadhimisha fungua hapa >>PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/03/27/kwanini-tarehe-ya-pasaka-inabadilika-kila-mwaka/