KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

Kwaresma ni nini?..Je! Kwaresma ipo katika Maandiko?..Na je ni lazima kufunga Kwaresma?, ni dhambi kuikatisha kwaresma? na je! ni dhambi kuishika kwaresma?


Neno Kwaresma limetokana na Neno la kilatini (Quadragesima) lenye maana “YA AROBAINI “… Kwahiyo siku ya 40 ndiyo inayoitwa Kwaresma..Kulingana na mapokeo ya, Madhehebu ya kikristo wanalitumia neno hilo kama kuwakilisha kipindi cha siku 40 cha mfungo kabla ya Pasaka.

Madhumini ya Mfungo huo ni kuwaandaa wakristo katika maombi, toba na kujinyenyekeza kwa ajili ya Pasaka ambayo itakuja baada ya siku hizo 40. Mfungo huo kulingana na mapokeo yao ni wa siku 40, lakini kiuhalisia ni zaidi ya siku 46..Kwasababu siku za jumapili huwa hazihesabiwi katika mfungo huo..Kwahiyo zinakuwepo jumapili 6 katika mfungo mzima..na kufanya Idadi ya siku za mfungo kuongezeka mpaka kufikia 46.

Mfungo huo pia unahusishwa na Bwana alivyofunga siku 40, akiwa jangwani, akijaribiwa na Ibilisi. Hivyo na wakristo wana jukumu la kufunga siku 40 kama Bwana alivyofunga.

JE KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

Jibu ni La! Hapana sehemu yoyote katika maandiko kuna sharti la kuitimiza Kwaresma..Hayo ni mapokeo..Na mapokeo yapo yaliyo mazuri na yaliyo mabaya..Mazuri ni yale ambayo hayakinzani na Neno la Mungu na mabaya ni yale yanayokinzana na Neno la Mungu na kuwafanya watu wawe wa kidini zaidi, kuliko kuwa wa Kiroho.

JE NI DHAMBI  KUISHIKA KWARESMA.

Katika Biblia ni wajibu wa kila Mkristo “kufunga na kusali”..Mambo hayo yanakwenda pamoja huwezi kusema unasali siku zote halafu hufungi hata mara moja, na pia huwezi kusema unafunga siku zote na husali hata siku moja. Kwahiyo Mfungo ni sharti kwa kila mwamini. Iwe ni mfungo wa wiki moja, wiki 2, siku 30, siku 40 au 50…Ni jambo la sharti. Na mfungo huo mtu auite kwa jina lolote iwe Kwaresma, jubilee, baragumu, au jina lolote lile ambalo mtu atapenda kuliita sio dhambi…

Kikubwa na cha msingi..Tendo lolote la kufunga halipaswi kuchukuliwa kidini..Kwamba mtu anafunga tu ili kutimiza sheria za dini yake, kama inavyofanyika leo. Haipaswi mtu kufunga halafu asiwe mwombaji…Wengi wanafunga lakini hata siku moja hawajawahi kutenga kusali hata lisaa limoja…huko ni kufunga kwa kidini ambako kuna matokeao madogo sana au kunaweza kusiwe na matokeo yoyote kabisa ikawa ni bure.

Hali kadhalika wakati wa Mfungo sio wakati wa kujichanganya na mambo ya kidunia, ni wakati wa kuwa katika utulivu wa roho na kujitesa nafsi, wakati wa kutubu kikweli kweli na wakati wa kuomba kwa bidii..Ni wakati wa kuongeza bidii sana katika mambo ya kiroho zaidi ya kimwili..Ndio maana unafunga kula..si wakati wa kuupendeza mwili ni wakati wa kuutiisha mwili.

Kwahiyo Mfungo huo unaoitwa Kwaresma kama hautafanyika kidini basi una matokeo makubwa sana kwa mhusika.

JE NI DHAMBI KUIKATISHA KWARESMA?

Mfungo mara nyingi ni kama Nadhiri, kabla ya kuanza kufunga mtu unaweka nadhiri kwamba unafunga siku 40, lakini ukisema unafunga halafu ndani ya mfungo huo unakuwa sio mwaminifu,  utakuwa unajipotezea muda tu wewe mwenyewe..Kama umeamua kufunga sharti umalize siku zote na kama huwezi basi usifunge…Maana utakuwa hujafunga kwa Imani, na biblia imesema tendo lolote lisilotokana na Imani ni dhambi (Warumi 14:23)

JE NI LAZIMA KUFUNGA KWARESMA?

Jibu ni la!..sio lazima kufunga wakati huo unaoitwa Kwaresma…lakini ni wajibu wa kila Mkristo kufunga..Kama hutafunga msimu huo ambao ni rahisi kueleweka na watu wengi…basi hakikisha unatafuta kipindi kingine katikati ya mwaka ambacho utafunga. Na kama ni mkristo kikweli kweli na si wakidini, basi utafunga nawe siku hizo hizo 40 au zaidi. Kwasababu ukilijua lile neno linalosema..

Matendo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”

Kwasababu kama mtu unayemwita wewe wa kidini anakushinda idadi ya siku za kufunga…hapo ni nani wa kidini?…wewe au yeye?..Jibu ni wewe?..kwasababu huwezi kufanya hata anachokifanya yeye..na bado unamwita wa kidini. Sharti ufanye kama yeye tena vizuri zaidi umpite ili uwe na sababu ya kumrekebisha, lakini kama huwezi kumzidi, yeye ndio anayepaswa akurekebishe wewe.

Bwana akubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JUMATANO YA MAJIVU NI TENDO LA KIMAANDIKO?

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

JE! NI DHAMBI KUIMBA WIMBO WA TAIFA?

JE KUJIUA NI DHAMBI?

YESU KWETU NI RAFIKI

MTINI, WENYE MAJANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Edmund
Edmund
2 years ago

Mbarikiwe kwa jumbe nzuri za kuinua IMANI NA UFAHAMU KWA WATU WAKE YESU KRISTO.Binafsi nimependa sana.amen