KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.

KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.

Kuota mtu amekufa au ndugu amekufa.


Wakati mwingine unaweza ukaota umefiwa na mzazi, au kaka au dada, au mtu wako wa karibu sana. Na ndoto hizi huwa zinakuja kwa uzito sana, kiasi kwamba unaposhtuka huamini kama kweli ilikuwa ni ndoto, kwasababu unaona kama tukio hilo lilikuwa ni halisi kabisa..unabaki kuishia  kumshukuru Mungu na kusema asante  kwa kuwa ilikuwa ni ndoto tu..

Ndoto kama hizi huwa zinawapata watu wengi, na kama haijawahi kukutokea, basi itakuja kukupata siku moja katika maisha.. Lakini fahamu kuwa ni Mungu  hapo anakukumbusha hatma ya maisha yako na ya ndugu zako itakavyokuwa..kwamba siku moja wataondoka duniani, sio lazima wafe kwa njia hiyo hiyo uliyoiona kwenye ndoto hapana bali inaweza ikaja kwa njia yoyote lakini lakini kitendo ni kile kile kifo..

Vilevile inaweza ikawa ni hivi karibuni, au isiwe hivi karibuni pengine baada ya miaka 5 au 10 au hata 50 lakini ujumbe ni ule ule, kifo kinakuja.

Hivyo ni wajibu wako kufanya mambo mawili makuu juu ya maisha ya ndugu zako angali wakiwa bado hai,

  • Kwanza: Ni kwa kuwahubiria habari njema za wokovu, wamrudie Mungu kama hawajaokoka..
  • Na pili: Ni kuwaombea maisha yao hapa duniani yawe ni ya kumcha Mungu na Mungu awaepusha na njama za Yule adui.

1Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka.”

Unaona Nabii Samweli hakuacha kuiombea Israeli japokuwa ilikuwa inamchukiza Mungu kwa sanamu zao, lakini alikuwa akidumu katika kuwaombea..aliwaombea kwa bidii sana, na akahesabu kwamba ni dhambi kuacha kuwaombea ndugu zake,…na pia akawa anawaonya..hata Musa naye kule jangwani ni mara nyingi Mungu alitaka kuwaangamiza wana wa Israeli kwa matendo yao maovu lakini kwa maombi ya Musa Mungu alighahiri mabaya yao.

Hivyo na wewe ikiwa upo ndani ya Kristo ni rahisi Mungu kusikia maombi yako na Mungu akawaweka katika mstari sahihi ikiwa utaendelea kuomba kwa bidii juu yao bila kukata tamaa, na vile vile Mungu atawaepusha na mabaya na njama nyingi za ibilisi ziliyopangwa kinyume chao, ikiwemo vifo ambavyo sio vya wakati.

Lakini kama upo nje ya Kristo, hakuna dua yoyote itakuwa rahisi kwa ndugu zako. Hivyo nakushauri umpe Bwana Yesu maisha yako leo, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha na kuwa tayari kumfuata yeye kwa moyo wako wote ili Bwana akuokoe kwanza wewe, ndipo iwe rahisi kusikia maombi yako kwa wengine.. Yesu sio wa watu wa dini Fulani tu, hata kama wewe ni muislamu, kimbilio lako ni YESU tu, wala hakuna mwingine..Yeye ndiye anayekuahidi uzima wa milele, yeye pekee ndio anayetoa faraja ya kweli ukiwa kwanza hapa duniani, na hata utakapofika kule..

Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo basi hapo

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa kuukamlisha wokovu wako.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312 jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Au jiunge Whatsapp hapa

https://chat.whatsapp.com/GBX2lWIcoCq8zmlnXJgaWQ

https://chat.whatsapp.com/GBX2lWIcoCq8zmlnXJgaWQ

Mada Nyinginezo:

Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?

KUOTA UPO UCHI.

Kuota unafanya Mtihani.

KUOTA UNAPAA.

USIKIMBILIE TARSHISHI.

KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Esther
Esther
2 years ago

Ameen tunafurahia mafundisho Yenu Mungu awabariki Sana

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ameen tunafurahia mafundisho Yenu Mungu awabariki Sana

Beatrice
Beatrice
3 years ago

Asante saana.. ubarikiwe