Ipi tofauti ya Ulawiti na Ufiraji (1Wakorintho 6:9)?

by Admin | 24 April 2024 08:46 pm04

Ulawiti na Ufiraji vina tofauti gani, kulingana na 1Wakorintho 6:9?


Jibu: Turejee…

1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, WALA WAFIRAJI, wala WALAWITI”

“Ulawiti” ni kitendo cha mwanaume kumwingilia mwanaume mwingine kinyume na maumbile… Na “Ufiraji” ni kitendo cha Mwanaume kumwingilia mwanamke kinyume na maumbile.

Mambo haya yote mawili ni machukizo makuu mbele za Mungu, na “wafiraji na walawiti” hawataurithi uzima wa milele sawasawa na maandiko hayo.

Kama wewe ni mwanaume na una mke jiepushe na Ufiraji!.. na kama wewe ni mwanamke na una mume kataa ufiraji, kama mwenzako anataka kukuacha kwasababu hiyo ya wewe kuukataa ufiraji, hapo yupo huru kuondoka!.. na wewe upo huru kuoa au kuolewa na mwingine mwenye kufanana na wewe, (asiyefanya mambo hayo na aliyeokoka)!

1Wakorintho 7:15 “Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika Amani”.

Neno “Ulawiti” limeonekana mara moja tu katika biblia na ni tendo baya kuliko ufiraji (Maana humu ndio wamo mashoga, jamii za wale watu wa Sodoma na Gomora).. Kwa ujumla Mkristo hapaswi kulawiti/kulawitiwa… kufira/kufirwa. Wote wafanyayo hayo, wana roho nyingine ndani yao, na sehemu yao itakuwa katika lile ziwa la moto.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

MSIWE NA UCHUNGU NAO!

Hapo ndipo, atakapompa Mungu Baba ufalme wake.

Fahamu maana 1Wakorintho 14:20  “Ndugu zangu msiwe watoto katika akili zenu;

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/04/24/ipi-tofauti-ya-ulawiti-na-ufiraji-1wakorintho-69/