Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18

Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18

Jibu: Tusome,

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.

Neno “Mbwa” kama linavyotumika hapo, linamaanisha “Mwanaume anayejiuza mwili wake”, kwa lengo la kupata fedha, kama vile mwanamke anayejiuza anavyojulikana kama Kahaba, vivyo hivyo mwanaume anayejiuza alijulikana kama “mbwa”.

Na kujiuza huko kuko kwa namna mbili. Namna ya kwanza ni mwanaume anayejiuza kwa wanawake, na namna ya pili, ni mwanaume anayejiuza kwa wanaume wenzake (yaani Hanithi). Makundi haya yote mawili yanajulikana kama “mbwa” kibiblia.

Hivyo Mungu alikataza kwa mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume anayejiuza mwili wake na kupata fedha, asizilete hizo fedha katika nyumba ya Mungu kama sadaka, kwaajili ya nadhiri, na si tu nadhiri bali pia kama sadaka!..kwani ni machukizo mbele zake.

Mithali 15: 8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.

Kwahivyo biblia inatufundisha kuwa Utakatifu ndio sadaka ya kwanza kwa Mungu wetu..Maana yake tusipokuwa watakatifu wa mwili na roho, na tukaenda kumtolea sadaka, huku hatutaki wala hatuna mpango wa kubadilika, bado ni wazinzi, bado ni waasherati, bado ni makahaba, bado ni wachawi, bado ni watu tuliojaa vinyongo na chuki..basi tujue kuwa sadaka ile tunayokwenda kuitoa ni machukizo makubwa sana kwa Bwana. Kwasababu kitu cha kwanza Bwana anachotafuta kwetu si PESA, wala SADAKA, bali anataka tuwe wakamilifu, anataka tupate Rehema..

Mathayo 9:13 “Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”.

Bwana Yesu mwenyewe alitupa ushauri mzuri, wa namna ya kumtolea Mungu..kwamba tujitakase kwanza kabla ya kwenda kumtolea yeye, ili sadaka yetu ikubalike na iwe na matokeo. Na kujitakasa huko sio kujitakasa leo, na kesho kurudia yale yale..bali ni kule kwa badiliko la kudumu ndani yetu..

Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.

Kinyume chake tukimtolea sadaka na huku hatuna mpango wa kuacha maisha yetu mabaya ya dhambi, tufahamu kuwa sadaka zetu hazitakubaliwa na zaidi ya yote hatutaurithi uzima wa milele..Na maandiko yanasema wazi kuwa waasherati na MBWA hawataurithi uzima wa milele.

Ufunuo 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya”

Bwana atubariki na kutujalia neema zake.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?

MTAWATUPIA MBWA NYAMA HIYO.

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?

Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments