SWALI: Bwana Yesu asifiwe naomba kufahamu maana ya hili andiko;
1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima”
JIBU: Kwa kawaida mtoto mchanga anakuwa kama mjinga, haelewi mambo mengi, anachofahamu ni kile tu kilichopo nyumbani, mambo mengine ya nje, hayajui, na ndicho kinachomfanya asijisumbue na hayo mengine, ambayo watu wazima wanayasumbukia,. Vivyo hivyo na Mungu anataka katika suala la uovu, tuwe hivyo. Kama wajinga, hatujui kinachoendelea, hatuna maarifa nayo, hatuwezi kuyaelewa. Na hiyo itatufanya tuwe salama.
Kwamfano ukiulizwa habari za nyimbo Fulani mpya za kidunia zilizotoka, huna taarifa nazo, Ukiulizwa habari za ligi za mipira, ni kama taarifa usizozielewa, ukisemeshwa na mambo ya kubeti, ni kama mtu anazungumza na wewe kwa lugha za mafumbo.
Ndio maana andiko hili linasema hivyo;
1Wakorintho 16:19b “…lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya”
Kutokujua kila kitu katika huu ulimwengu sio dhambi, na wala hilo halitakuzuia uishi vema. Hivyo tunapaswa tuchuje, ni nini kinatufaa na kipi kisichotufaa, Vile visivyotufaa tuviweke kando, tuwe watoto katika hivyo, lakini vile vitujengavyo, ambalo ni NENO LA MUNGU, basi tuwe watu wazima. Tulijue sana hilo kwasababu ndio uzima wetu ulipo.
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia?
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13)
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
Je biblia inatufundisha tuwe wapole kiasi? (Wagalatia 5:22-23)
Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?
Rudi nyumbani
Print this post