MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE.

MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE.

Jina la Bwana YESU KRISTO, Mkuu wa uzima, libarikiwe.

Karibu tujifunze biblia, neno la Mungu wetu lililo taa na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105)

Biblia inatufundisha kuwa TUMTAKE BWANA na NGUVU ZAKE.

Zaburi 105: 4 “MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE, Utafuteni uso wake sikuzote”. 

Wengi tunaishia “Kuzitaka tu nguvu za Bwana” …. lakini biblia hapa inatufundisha tumtake Bwana pamoja na nguvu zake, maana yake mambo hayo mawili yanaenda sambamba…

Unaweza kuwa na nguvu za Bwana, lakini usiwe na Bwana kabisa!, utauliza kwa namna gani?.

Bwana Yesu alisema, wengi watakuja siku ile na kusema Bwana hatukufanya miujiza mingi kwa jina lako?, lakini yeye atasema “sikuwajua kamwe”.

Mathayo 7:22  “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?.

23  Ndipo nitawaambia dhahiri, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Nataka uone hapo anaposema “sikuwajua kamwe”.. Neno “kamwe” maana yake ni kwamba hajawahi kabisa kuwa na mahusiano nao, katika kipindi chote na maisha yao..maana yake tangu wakiwa duniani Bwana hakuwajua watu hao, ingawa walikuwa wanazo nguvu za Mungu zikitembea nao,  walikuwa na nguvu za Mungu za kutoa pepo, za kufanya miujiza mingi, lakini hawakuwa na Mungu katika maisha yao.

Sasa biblia inatufundisha tumtake “Bwana na Nguvu zake”, cha kwanza tumatake yeye Bwana, halafu cha pili ndio kiwe nguvu zake!.

Sasa tunamtakaje Bwana na tunampataje Bwana?..Tunampata Bwana kwa kuyafanya mapenzi yake.

Na mapenzi ya Mungu ni yapi?

1Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;

4  kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;

5  si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Na tunatakaswa kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo, ambapo Imani hiyo inazaa toba na ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO kwaajili utakaso wa dhambi (Matendo 2:38) . Kwa kufanya hayo basi utakuwa umemtaka Bwana, na yeye ataingia katika maisha yako, na atadhihirisha neema yake kwako pamoja na nguvu zake.

Lakini usitangulize kuzitafuta nguvu za Mungu na huku yeye hayupo nawe!.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

JINSI YA KUSIMAMA NA KUFUNDISHA/ KUHUBIRI

USIMPE NGUVU SHETANI.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

KUOTA UPO KANISANI.

Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments