Je biblia inatufundisha tuwe wapole kiasi? (Wagalatia 5:22-23)

Je biblia inatufundisha tuwe wapole kiasi? (Wagalatia 5:22-23)

Swali: Biblia inatufundisha katika Wagalatia 5:23  kuwa “tuwe wapole kiasi”, sasa napenda kujua mtu utakuwaje mpole kiasi.

Jibu: Tusome,

Wagalatia 5:22  “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23  UPOLE, KIASI; juu ya mambo kama hayo hakuna sharia”.

Hapa biblia haisemi kuwa tunda la Roho Mtakitifu kuwa ni “Upole kiasi” kana kwamba “upole unapaswa uwe na kiasi”…. La! Bali inasema tunda la Roho ni “Upole”, halafu “Kiasi”… hayo ni maneno mawili yaliyotengenishwa na alama ya mkato.

Maana yake “Upole” ni kitu kingine na “Kiasi” ni kitu kingine. Ikiwa na maana kuwa Tunda la Roho “Upole ulio wote” na sio upole kiasi.

Biblia inatufundisha tuwe watu wapole kama Hua (Njiwa).

Mathayo 10:16  “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua

Hua ni ndege mpole sana ndio maana Roho Mtakatifu alitumia umbile la Hua kushuka juu ya Bwana Yesu wakati ule alipobatizwa (Mathayo 3:16)... Na maandiko yanazidi kutufundisha kuwa Bwana Yesu ni Mpole..

Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.

Soma pia, Mathayo 11:29, utaona sifa hiyo ya Bwana ya upole ikitajwa..

Na sisi pia ni lazima tuwe na sifa hiyo ya “Upole” kama ishara mojawapo ya kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu… shetani kaligeuze Neno hili la Upole na kuweka “Upole kiasi” ili kuchochea ubaya ndani ya watu.. Kwamba ni vizuri kuwa wapole lakini tusiwe wapole sana, tuwe wapole tu kiasi!. Huo ni uongo wa adui!.

Na kumbuka kuna tofauti ya “upole” na “unyonge”. Biblia haitufundishi kuwa wanyonge, bali kuwa wapole, Mtu mpole ni yule ambaye ana uwezo wote wa kutumia ukali lakini hautumii!, kama alivyokuwa Bwana Yesu… Lakini mnyonge ni yule anayekuwa analazimika kuwa hivyo mpole kutokana tu na mazingira..na akitoka katika hayo mazingira basi tabia yake ya ubaya na ukali usio na maana na vurugu inajidhihirisha.

Bwana atusaidie .

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Upole ni nini?

KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?

BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments