HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO UTAKAPOKUWAPO NA MOYO WAKO.

HAZINA YAKO ILIPO, NDIPO UTAKAPOKUWAPO NA MOYO WAKO.

Hakuna namna utautenganisha “Moyo” na “hazina”.. vitu hivi vinaenda pamoja!.(ni sawa na miguu na mwili,..mahali miguu ilipo na mwili upo, miguu haiwezi kuwa mahali pengine na mwili mahali pengine) Vile vile Moyo wa mtu na hazina yake, vinaenda pamoja…Pale mtu alipojiwekea hazina, ni lazima (akili yake yote na fikra zake na hisia zake na mawazo yake yatakuwa huko).

Ndio maana mtu aliyejiwekea hazina kubwa ya mali za kidunia, halafu mali zile zikapotea zote ghafla, ni rahisi mtu huyo kuchanganyikiwa au kupoteza maisha maisha kabisa!.

Kwanini?..Kwasababu Moyo wake wote (fikra, mawazo, akili, malengo, uzima, hadhi) vilikuwepo katika mali zile, na sasa hana tena!, hata maisha kwake yanakuwa hayana maana tena!. Ndivyo ilivyo, kwamba Moyo siku zote unafuata hazina ilipo!, na unaishi kutokana na hazina mtu alizonazo. Ndivyo moyo wa mtu ulivyoumbwa!..

Vile vile mtu anayejiwekea hazina mbinguni, ni lazima fikra zake, mawazo yake, akili yake, malengo yake yote yatakuwa kule mbinguni hazina yake ilipo.

Sasa Bwana Yesu alitufundisha kanuni ya kuielekeza Mioyo yetu mbinguni, kwamba si kwa kuomba tu! Bali kwa kujiwekea hazina kule mbinguni,..kwanini?…kwasababu tutakapojiwekea hazina kule juu mbinguni basi mioyo yetu (yaani fikra, fahamu, akili, mawazo na hisia) zitaelekea kule Mbinguni, bila shuruti!.

Sasa swali, tunajiwekeaje hazina juu mbinguni?.. yeye mwenyewe (Bwana Yesu) alitufundisha kanuni katika Luka 18:18-22

Luka 18:18 “Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?

19  Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu.

20  Wazijua amri; Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

21  Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu

22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, NAWE UTAKUWA NA HAZINA MBINGUNI; kisha, njoo unifuate”.

Na tena anarudia maneno kama hayo hayo katika Luka 12:32-34

Luka 12:32  “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.

33  Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, AKIBA ISIYOPUNGUA katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.

34  KWA KUWA HAZINA YENU ILIPO, NDIPO ITAKAPOKUWAPO NA MIOYO YENU”.

Umeona?.. Kumbe kanuni ya kujiwekea hazina mbinguni ni kumtolea Mungu!..

Kwanini?.. Kwasababu tunapomtolea Mungu vile tulivyo navyo, mawazo yetu yatakuwa siku moja kwenda kupata thawabu mbinguni!, fikra zetu zitakuwa siku moja kwenda kuona miji mizuri tuliyoandwaliwa, mawazo yetu yatakuwa siku moja kwenda kuvikwa taji……hivyo muda wote tutakuwa tunafakari tu yaliyo ya juu na huko ndiko mioyo yetu itakapokuwepo!.

Ndio maana utaona watu wanaojitoa kwa Mungu kuanzia miili yao, mpaka mali zao, muda wote wanawaza unyakuo utakuwa lini?, muda wote wanawaza Kristo anakuja lini?.. ni kwanini wanakuwa hivyo?, si kwamba wanajilazimisha kuwa hivyo, ni kwamba tayari mioyo yao ipo mbinguni kwasababu wamejiwekea hazina huko.

Hii ni kanuni rahisi kabisa ya kuhamisha mioyo yetu kutoka kutafakari MAMBO YA CHINI na kuanza kutafakari MAMBO YA JUU!.

Ukitaka uwe mtu wa kutafakari mambo ya mbinguni sana, mtolee Mungu kuanzia muda wako, akili yako, mwili wako, ufahamu wako na hata vitu vyako!.. Hapo moyo wako wenyewe tu utaanza kuelekea mbinguni bila hata kutumia nguvu nyingi!,. Utajikuta tu unaanza kutamani kumwona Yesu, utajikuta unatamani ile siku ya mwisho ifike n.k

Laakini kinyume chake usipofanya hivyo na ukajitumainisha katika kujiwekea hazina katika mambo ya ulimwengu, basi fahamu kuwa moyo wako utaelekea tu katika mambo ya ulimwengu hata kama hupendi!.

Wakolosai 3:2 “Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Hazina za gizani ni zipi? (Isaya 45:3).

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

UKIOKOKA, JIANDAE KUPITISHWA USIPOPATAZAMIA.

Yeshuruni ni nani katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments