Fahamu Maana ya;
Mithali 18:18 Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Kupiga kura ni Moja ya njia ambayo ilitumika kuleta suluhisho lenye utata, na wakati mwingine kuchagua viongozi/wamiliki. Pitia hapa ujue zaidi kuhusu kura zilivyopigwa zamani za biblia…>> Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;
Na Mungu wakati mwingine aliingilia kati na kuleta majibu yake sahihi kwa kupitia njia hiyo. Kwamfano wakati ule Yona anamkimbia Mungu, Hali ilipochafuka kule baharini, utaona wale watu walipiga kura, ili kujua sababu ya mambo yale ni nani na Ile kura ikamwangukia Yona.
Mitume wa Bwana baada ya kuomba, kuhusu mrithi wa nafasi ya Yuda wakapiga kura katika ya wale wanafunzi wawili, nayo ikamwangukia Mathiya, na likawa kweli ni chaguo la Mungu.(Matendo 1:15-19),
Hata wakati wa nchi ya Israeli kugawanywa . Kura zilitumika kuamua nani akae wapi, na nani arithi wapi (Hesabu 26:55).
Hivyo kupiga kura ilikuwa ni mojawapo ya njia kuleta jibu lisilokuwa na upendeleo. Au lililoegemea upande Fulani mmoja. Na kwa kufanya hivyo malalamiko mengii yalikomeshwa kwasababu maamuzi hayakuamuliwa na upande wowote ule.
Ndio maana ya hili andiko
Mithali 18:18
[18]Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
Hata kipindi Cha sasa njia ambayo hutumiwa kuchagua viongozi wengi ulimwenguni Huwa ni ya kura. Isipokuwa hii siyo ya kurusha SHILINGI, au kete angani inayomwangukia mmojawapo ndio anakuwa kiongozi..hapana Bali ni kuruhusu Kila mmoja kutia maoni yake..Kisha zinahesabiwa na yule mwenye nyingi hupewa. Na hivyo hakuna malalamiko.
Tofauti na Ile mtu atawadhwe tu Moja Kwa moja kuwa kiongozi, Hiyo huleta ukakasi mwingi.
Hivyo ni kutufundisha kua Bwana anaouwezo wa kuingilia kura zipigwazo na kuleta majibu yake sahihi..hususani pale anaposhirikwa Kwa maombi, na kama hakusema Kwa njia nyingine ya Moja Kwa moja.
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
MKUU WA ANGA.
Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
Rudi nyumbani
Print this post