Heshima ni nini kibiblia?

by Admin | 16 May 2024 08:46 pm05

Heshima ni kitendo cha kumpa mtu hadhi yake, au uthamani wake anaostahili. Kwa kawaida kila mwanadamu anastahili heshima. Na hivyo kama mwamini huna budi kujua jinsi ya kuigawanya heshima kulingana na mtu husika. Kwasababu ukosefu wa heshimu, kwanza ni zao la kiburi (Mithali 15:33), lakini pia hukuondolea Baraka na kibali  popote pale uendapo. Lakini pia ukitoa heshima isiyompa mtu ni kosa pia.

Warumi 13:7  Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima

Heshima kwa Mungu ipo wapi?

  1. Ipo katika kuliamini na kuliishi Neno lake: Si katika kulipamba jina lake, na huku hufanyi anayokuambia. Alisema. Luka 6:46  Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47  Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.
  2. Ipo katika uaminifu katika  utoaji: Mithali 3:9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote
  3. Ipo katika ibada :  Anayestahili kuabudiwa, kusujudiwa, kupigiwa magoti, kuhimidiwa ni Mungu tu peke yake, na wala si mwanadamu au kiumbe kingine pamoja naye, heshima hii inamuhusu yeye peke yake. Ufunuo 4:11 “ Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa”

Heshima kwa Wazazi ipo wapi?

  1. Kuwasaidia. Biblia inasema kuwaheshimu wazazi ni pamoja na kuwasaidia kimahitaji (Mathayo 15:1-7)
  2. Kuwasikiliza na kushika maagizo yao: Mithali 1: 8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

Heshima kwa Viongozi wako wa kiroho ipo wapi?

Kutii maelekezo yao.

Waebrania 13:17  Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

Heshima kwa watoto ipo wapi?.

Kutowakwaza,

Waefeso 6:4  Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

Heshima kwa Viongozi wa nchi.

Kutenda agizo lao.

Warumi 13:1  Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2  Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu

Heshima kwa Mabwana ipo wapi?

Kuwatumikia kwa uaminifu na adabu. (Waefeso 6:5-8)

Hivyo kwa hitimisho, ni kwamba kila mwanadamu anastahili heshima, haijalishi, tajiri, au maskini, mrefu au mfupi, mgonjwa au mzima, mwenye elimu au asiye na elimu, bwana au mtumwa, ameokoka au hajaokoka. Wote ni agizo tuheshimiane.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?

CHUJIO HILI NI LA AJABU SANA!

JIWE LILILO HAI.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/05/16/heshima-ni-nini-kibiblia/