Majumbe ni watu gani? (Mwanzo 36:15).

by Admin | 28 June 2024 08:46 pm06

Jibu: Turejee..

Mwanzo 36:15 “Hawa ndio MAJUMBE wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; JUMBE Temani, JUMBE Omari, JUMBE Sefo, JUMBE Kenazi,

16 JUMBE Kora, JUMBE Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio MAJUMBE, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada”.

Jumbe/Majumbe ni “WAKUU WA KOO” (machifu),

Majumbe walikuwa ni watu wenye heshima katika ukoo, na walijulikana sana katika nchi yote… na pia Majukumu yao yalikuwa ni kutatua migogoro ya kifamilia, na migawanyo ya ardhi kwa familia.

Katika biblia majumbe waliokuwa maarufu ni Majumbe wa wana wa Esau, (Hawa ndio waliokuwa Majumbe maarufu na wenye heshima kuliko Majumbe wa kabila nyingine za watu).. Jamii yao iliwapa heshima Majumbe hawa kiasi kwamba wakajulikana mpaka nje ya mipaka.

Kutoka 15:14 “Kabila za watu wamesikia, wanatetemeka, Wakaao Ufilisti utungu umewashika.

15 Ndipo MAJUMBE WA EDOMU wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka”.

Sehemu nyingine katika biblia zilizotaja Majumbe ni pamoja 1Nyakati 1:51-54, Esta 1:3, Esta 9:3

Lakini pamoja na kwamba “Majumbe wa Esau” walikuwa maarufu na waliojulikana sana na wenye heshima, lakini kutoka huko hakutoka “MKUU WA UZIMA (YESU KRISTO), lakini badala yake kutoka katika Ukoo mdogo sana, (wa Majumbe ya Yuda), alitoka Mwokozi wa ulimwengu, Haleluya!!..

Mathayo 2:5 “Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6  Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, HU MDOGO KAMWE KATIKA MAJUMBE WA YUDA; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli”.

Je umemwamini Bwana YESU?.. Kama bado fahamu kuwa tunaishi majira ya kurudi kwake, na ule mlango unazidi kuwa mwembamba kila siku na ile njia ya upotevuni inazidi kuwa pana kwa kadiri muda unavyozidi kwenda, hivyo usikawie kusimama katika wokovu, muda umebaki mchache sana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

JE! UNA MHESHIMU MUNGU?

Heshima ni nini kibiblia?

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/06/28/majumbe-ni-watu-gani-mwanzo-3615/