TUJIHADHARI NA KUKANWA!.

by Admin | 22 July 2024 08:46 pm07

Mathayo 10:33 “Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni”

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia.

Hebu tulitafakari kwa upana kidogo  hili neno “kukanwa”.

Kukanwa ni ile hali ya kukataliwa na mtu unayemjua, unayetembea naye daima, uliyeweka matumaini yako kwake, mnayekubaliana  au uliye na mahusiano naye ya karibu”

Na ipo tofauti ya “kukana na kusaliti”…kwa urefu juu ya tofauti ya maneno haya mawili fungua hapa 》》Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?

Sasa Bwana YESU anasema kuwa tukimkana mbele ya watu naye atatukana mbele ya Baba yake kule mbinguni.

Hebu tengeneza unafika kule, halafu unakanwa na yule ambaye ulikuwa unaona anatembea na wewe kila siku, anakuponya, anakulinda, ukiliita jina lake maajabu yanatokea, pepo zinatoka na miujiza mingi inafanyika.

Halafu huyu huyu ambaye ulipokuwa duniani alikuwa haonyeshi dalili ya kukukataa lakini unafika kule anakukana anasema hakujui!..ni jambo gumu sana kuamini!.

Lakini ndivyo itakavyokuwa siku ile..

Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Hatuna budi kukaza mwendo daima na kila siku tukihakiki ni lipi limpendezalo Bwana (Waefeso 5:10).

Mtume Paulo ijapokuwa alikuwa na wingi wa mafunuo lakini alisema maneno haya..

1 Wakorintho 9:26 “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;

27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.

Na pia alisema…

Wafilipi 3:12 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.

13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MFALME ANAKUJA.

JINA LAKO NI LA NANI?

UWEZA WA MUNGU NJE YA WAKATI.

Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)

JE UNAMHUBIRI KRISTO KATIKA KWELI YOTE?.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/22/tujihadhari-na-kukanwa/