Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)

Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)

Kulabu ni nini katika biblia?


Kulabu ni aina ya ndoano, tofauti na ile ya kuvulia samaki hii ni ile inayotumiwa kushikilia vitu, kama vile mapazia, mashuka, nguo n.k., tazama picha juu uone mfano wa kulabu za mapazia,

Na ndio zilikuwa zinatumika katika kushikilia nguo za ua wa hema ya kukutania.

Kutoka 26:37 “Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; KULABU ZAKE ZITAKUWA ZA DHAHABU; nawe utasubu matako ya shaba matano kwa ajili yake”.

Kutoka 27:9 “Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia;

10 na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na matako yake ishirini, matako yake yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha”.

Soma pia Kutoka 27:11,17, 36:36, 38:10,11,12.

Lakini pia Mungu amelitumia  Neno hili, kama mfano kwa watu wanaokaidi maagizo yake, kwamba atawatia kulabu/ndoano hiyo puani mwao.

Na kama tunavyojua, wanyama wanaotiwaga kulabu kama hizi puani mwao, huwa wanatii kwa lolote watakaloamrishwa, popote watakapopelekwa watakwenda tu haijalishi ni wakorofi kiasi gani.

2Wafalme 19:27 “Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako unayonighadhibikia.

28 Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia”.

Maneno haya aliyarudia tena katika Isaya 37:28

wa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijiaHivyo na Mungu pia anaweza kutitia kulabu na kutulazimisha kwenda mahali ambapo sisi hatutaki, kwa kosa moja tu la kuasi maagizo yake. Mifano kama hiyo tunaiona kwa wafalme wengi wa Israeli wengine walichukuliwa utumwani Babeli, wengine na walichukuliwa na maadui zao. Hivyo na sisi tusipokuwa watiifu kwa Mungu atatutia kulabu.

Bwana atusaidie tusifikie viwango hivyo.

Shalom.

Mistari mingine inayoelezea Neno hili, ni hii;

Ayubu 41:1 “Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?

2 Je! Waweza kutia kamba puani mwake? Au kutoboa taya yake kwa kulabu”?

Ezekieli 19:4 “Mataifa nao wakapata habari zake, akanaswa katika rima lao, wakamchukua kwa kulabu mpaka nchi ya Misri”.

Ezekieli 19:9, 29:4

Amosi 4:2 “Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajilia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana”.

Tazama maana ya maneno mengine chini;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Kuchelea ni nini?(2Wakorintho 11:3)

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments