by Admin | 25 July 2024 08:46 am07
Jibu: Turejee..
1Wakorintho 2:2 “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa”
Haya ni maneno ya Mtume Paulo aliyowaambia watu wa kanisa la Korintho… sasa tunaweza kuyaweka katika lugha rahisi namna hii…. “Nilipokuja kwenu (ninyi Watu wa Korintho) nilikusudia kufahamu yale mnayoyajua kumhusu YESU KRISTO, ambaye amesulubiwa na si jambo lingine lolote”.
Maana yake Paulo alitaka kuelewa ni nini Wakorintho wanaelewa kumhusu YESU aliyesulubiwa, hicho tu ndicho alicholenga kujua, na hakutaka kujua mambo mengine..
Kwanini alitaka kujua ufahamu wao kuhusu YESU?…
Ni kwasababu alijua kama wakimfahamu YESU kama inavyopaswa kufahamika, basi Imani yao itakuwa katika msingi thabiti.. Lakini kama wakimfahamu Yesu kwa ushawishi wa Maneno, basi Imani yao itakuwa katika hekima za kibinadamu.
1Wakorintho 2:1 “Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.
2 Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.”
Vile vile kama watamfahamu YESU wa ishara na miujiza tu, basi Imani yao itakuwa katika miujiza na ishara kama wale Wasamaria (Yohana 6:26) na si katika Imani thabiti ya YESU ALIYESULIBIWA
Lakini kama wakimfahamu YESU kama Mwokozi aliyesulibiwa kwaajili ya makosa yao na dhambi zao, basi Imani yao itakuwa thabiti, na yenye uhakika.. Itakayowapelekea kuungama dhambi, na kutafuta kuyafanya mapenzi ya Mungu, jambo ambalo ni msingi sana, na ambalo ndio tiketi ya kumwona Mungu (Mathayo 7:21-23)
Hivyo na sisi kilicho kikubwa na cha Msingi ni kuishikilia ile Imani ya Msingi (ambayo ndio Imani mama), ambayo inatupeleka/kutusukuma kujitakasa na kujiepusha na uchafu(dhambi).
Bwana atusaidie, na Bwana atubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?
Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?
MSINGI WA NYUMBA YA MUNGU, NI JINA LA MUNGU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/25/nini-maana-ya-naliazimu-nisijue-neno-lolote-kwenu-1wakorintho-22/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.