Fahamu mana ya Zaburi 48:14 Yeye ndiye atakayetuongoza

by Admin | 26 July 2024 08:46 am07

SWALI: Ipi tafsiri ya Zaburi 48:14 ?

[14]Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele  Yeye ndiye atakayetuongoza.


JIBU: Mwandishi anajivunia sifa ya Mungu wao wa milele. kwamba ndiye atakayewaongoza.

Akiwa na maana atayewaongoza katika mambo yao yote, kwamba kamwe hawezi kuwaacha, atakayewaongoza njia sahihi ya uzima, njia sahihi ya kupigana vita, ya kujenga na kupanda.

Ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli. Mungu alikuwa nao jangwani kwa nguzo ya moto na wingu kuwaongoza, aliwapelekea malaika wake kuwalinda, aliwafundisha namna ya kupata faida katika shughuli zao, akawainulia na waamuzi, pamoja na wafalme na manabii kuwachunga na mwisho akawaletea mkombozi, ambaye ndio ukamilifu wa yote. Kuonyesha wema wake na kiu yake ya kuwaongoza  watu wake.

Hata sasa, sifa yake ndio hiyo hiyo, ndio maana na sisi tuna ujasiri wa kusema…

‘Yeye ndiye atakayetuongoza’.Sio tu kwa wakati huo, bali mpaka siku ya kufa kwetu.

Alipokuja mwokozi hakutuacha hivi hivi kama mayatima, bali alituachia msaidizi ambaye anatuongoza na kututia katika kweli yote, ndiye Roho Mtakatifu.

Yohana 16:13

[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Bwana akubariki.

Je umempokea Yesu?  Kama bado ni nini unasubiri ? Fungua hapa kwa mwongozo wa sala  ya toba ya imani. >>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/07/26/zaburi-4814-yeye-ndiye-atakayetuongoza/