Bwana YESU alibatizwa na umri gani?

by Admin | 2 August 2024 08:46 am08

Jibu: Umri kamili ambao Bwana YESU alikuwa nao wakati anabatizwa na Yohana katika mto Yordani, ni miaka thelathini (30).

Tunalithibitisha hilo katika Luka 3:21-23..

Luka 3:21 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

22  Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

23  Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, ALIKUWA AMEPATA UMRI WAKE KAMA MIAKA THELATHINI”

Sasa kwanini Bwana Yesu abatizwe ukubwani na si utotoni?…Jibu rahisi ni kwamba alikuwa anatupa kielelezo, kwamba mwamini anapaswa abatizwe wakati ambao yeye mwenyewe kajitambua na kuona sababu zote za kubatizwa kwa hiari yake mwenyewe na si kwa kuamuliwa.

Kwa uthibitisho huo basi ni wazi kuwa “ubatizo wa utotoni” si sahihi.. Huenda waliosimamia ubatizo huo walikuwa na nia njema, lakini bado Neno la Mungu litabaki kuwa lile lile, kuwa ubatizo wa utotoni sio sahihi kimaandiko, hivyo hatuna budi kuweka mitazamo yetu pembeni, na mawazo yetu, na mapokeo yetu, na kulisimamisha Neno la Mungu.

Hakuna mahali popote katika maandiko, watoto walibatizwa, au watu walibatizwa kwa maji machache… Zaidi sana maandiko yanatuonyesha watu walisafiri kwenda mpaka Ainoni alipokuwa akibatiza Yohana, kwasababu kule kulikuwa na MAJI TELE.

Yohana 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na MAJI TELE; na watu wakamwendea, wakabatizwa”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?

Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/08/02/bwana-yesu-alibatizwa-na-umri-gani/